Na Shani Amanzi, Chemba.

OFIS Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Chemba mkoani Singida Mwatumu Doso amewataka wanawake watumie vema fursa wanazozipata kwa kuwa wao ndiyo kioo katika jamii hasa katika nyadhifa mbalimbali ikiwemo za uongozi wanazopewa katika jamii.

Doso ametoa kauli hiyo kwenye ufungaji wa Mafunzo ya Uongozi yaliyofanyika kwa siku mbili kuanzia Juni 19 hadi Juni ,mwaka huu wilayani Chemba.Mwatumu amesema "kwa muda wa miongo kadhaa iliyopita,wanawake wametokea kuwa wenye juhudi nyingi katika masuala ya jamii zao.

"Lakini kumekuwepo na changamoto mbalimbali zinazowakwamisha ndiyo maana Serikali pamoja na Sekta Binafsi zinajitahidi kuwashika mikono wanawake ili wapate maendeleo."

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la UFUNDIKO (Ufundi na Uhandisi Kongwa) Saidi Panga amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wanawake katika uongozi bora na kujua majukumu yao ya msingi katika Uongozi na kuweza kujua uhusiano uliopo kati ya Viongozi na Wanaongozwa.

"Uongozi usio rasmi mahali popote una umuhimu wake na viongozi wanapotenda shughuli zao hivyo kiongozi anawajibu wa kutambua kuwepo kwa taasisi zisizo rasmi."Na kufanya kila njia kuzitumia katika kufanikisha malengo yake au ya Halmashauri kwa hiyo ni wajibu wa Viongozi kutumia njia sahihi za Uongozi,"amesema Panga.

Katika mafunzo hayo yalishirikisha vijiji 12 ambavyo ni Tandala,Kidoka,Mondo,Goima ,Kilema Balai,Lahoda,Lalta,Jangalo,Kwamtoro,Gwandi,Mrijo Chini na Makorongo ambapo katika kila kijiji kilileta wahusika wanawake watano ambapo wapo kwenye makundi matatu likiwemo kundi la kwanza wahusika watatu kutoka kamati ya maji ya kijiji ,kundi la pili ni Muuguzi wa Zahanati na kundi la tatu Kiongozi mmoja wa kijiji.
Picha ya pamoja ya Washiriki wa Mafunzo wakiwa na Mwezeshaji wao Mkurugenzi wa Shirika la UFUNDIKO (Ufundi na Uhandisi Kongwa) Saidi Panga .


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...