WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wasikubali kuchonganishwa na
kwamba Serikali haiongozwi kwa misingi ya kidini bali imeziachia taasisi
za kidini zifanye kazi kwa kuzingatia Katiba , Sheria za nchi na
malengo yaliyokusudiwa katika uanzishwaji wake.
Aliyasema
hayo jana jioni (Jumamosi, Juni 9, 2018) alipozungumza na viongozi na
wananchi wa Mkoa wa Mwanza baada ya kushirikiana nao katika futari
aliyowaandalia. Shughuli hiyo ilihudhuriwa na waumini wa dini
mbalimbali.
Waziri
Mkuu alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wake wanaishi
kwa amani na utulivu, jambo litakalowawezesha kufanya shughuli zao
kikamilifu, hivyo wasikubali kuchonganishwa kwa misingi yoyote.
“Nawaasa
viongozi wa dini msikubali kutumia makundi mengine nje ya taasisi zenu
kwa ajili ya kuwazungumzia masuala yenu kwa sababu watawachonganisha na
Serikali ambayo haipo kwa ajili ya kugombana na taasisi yoyote,”
alisisitiza.
Waziri
Mkuu alisema jukumu kubwa la taasisi za kidini ni kuhakikisha
wanawalinda waumini wao pamoja na kuwaongoza kwa kuwapa mafundisho mema
yanayompendeza Mwenyezi Mungu, ambayo yatawawezesha kuishi kwa amani .
Alisema
misingi ya amani na utulivu ikiwa pamoja na mshikamano walionao
wananchi umesababisha Tanzania kupata heshima kubwa dunia kote, hivyo ni
vema kila mwananchi ahakikishe suala la kudumisha amani linapewa
kipaumbele.
Pia
Waziri Mkuu alisema amefurahi sana kujumuika na wananchi wa Mkoa wa
Mwanza katika futari hiyo, ambapo aliwapongeza kwa kukamilisha uundaji
wa kamani za amani kuanzia ngazi ya kata hadi mkoa.
Awali,
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw. John Mongella amlishukuru Waziri Mkuu kwa
ukarimu wake kwa kuwaalika wakazi wa Mwanza katika hafla hiyo, ambapo
alisema Mwanza ni kitovu cha amani kwa kanda ya Ziwa na nchi za Maziwa
Makuu. T
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...