WAZIRI wa Afya,maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameweka jiwe la msingi katika Kituo cha Afya Mdemu kilichopo Wilayani Bahi Jijini Dodoma baada ya kuridhishwa na ujenzi huo.

Akizungumza wakati wa kuweka jiwe hilo la msingi Waziri Ummy alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imefanya kipaumbele maboresho mbalimbali hususan katika sekta ya afya nchini.

“Nilipofika hapa mwaka 2016 niliona wanawake wajawazito wanalala kwa kubanana na wengine wanafariki kwa uzazi pingamizi hivyo nikaona tuanze kujenga vyumba vya upasuaji wa dharura nchini ikiwemo wodi ya wanawake wajawazito ili kuokoa Maisha ya mwanamke na mtoto anapojifungua ” alisisitiza Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy alisema kuwa mpaka sasa wilaya ya Bahi imefikia asilimia 98 ya wanawake wajawazito kujifungulia katika vituo vya afya amabapo Kitaifa inaonesha katika kila wanawake 100 wanawake 51 ndo hijifungilia kwenye vituo vya afya.Vilevile Waziri Ummy amesema kuwa Juhudi za Serikali katika kuokoa vifo vya wakina mama wajawazito Kijijini Mundemu atawapatia gari ya kubebea wagonjwa kwa ajili ya rufaa kutoka kituo kituoni hapo kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Bi. Benadertha Januari amesema kuwa wamefanikiwa kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kutoka vifo 4 mwaka 2015 mpaka vifo 3 mwaka 2017 na vifo vya watoto chini ya miaka 5 kutoka 50 mwaka 2015 mpaka kufikia vifo 12 2017.Aidha Bi. Januari amesema kuwa wamefanikiwa kukusanya chupa za damu salama 1640 kati ya chupa 2216 ya malengo waliojiwekea ambayo ni sawa na asilimia 74 kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Juni mwaka huu.

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Kata ya Mundemu Bw. Reuben Ntiruka amesema kuwa Kituo cha afya Cha Mundemu kinapokea rufaa ya kutoka Zahanati 21 za vijiji vitatu ambayo idadi ya walengwa wake ni wananchi 9103.Mbali na hayo Bw. Ntiruka ameiomba Serikali kuijengea Kituo hicho Uzio ,nyumba za watumishi, kuongeza idadi ya watumishi pamoja gari ya kubebea wagonjwa kwani ndio changamoto kubwa zinazoikumba Kituo hicho cha afya.
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akiweka jiwe la msingi Mradi wa ukarabati na uboreshwaji katika Kituo Cha Afya Mdemu kilichopo Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma leo.kulia ni Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Mzee na Mbunge wa Bahi Bw. Omari Baduel.
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikagua majengo ya wodi ya wajawazito,jengo la upasuaji wa dharura ,Mochwari ,sehemu ya kuchomea taka na maabara katika Kituo Cha Afya Mdemu kilichopo Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma kabla ya kuweka jiwe la msingi leo. 
 Mbunge wa Jimbo la Bahi Bw. Omari Baduel akiongea na wanakijiji wa kata ya Mdemu hawapo pichani wakati wa uwekaji jiwe la msingi katika kituo cha Afya Mdemu wilayani Bahi  jijini Dodoma, kushoto waliokaa ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na anayefuata ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi Bi. Elizabeth Kitundu 
 Baadhi ya wanakijiji waliojitokeza kumsikiliza na kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi katika Kituo cha afya Mdemu uliofanywa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wilayani Bahi  jijini Dodoma.
 Baadhi ya wanakijiji waliojitokeza kumsikiliza na kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi katika Kituo cha afya Mdemu uliofanywa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wilayani Bahi  jijini Dodoma.
Mafundi wakiwa katika hatua ya mwisho ya kumalizia jengo la Mochwari lilipo katika Kituo cha Afya Mdemu Wilayani Bahi Mkoa Dodoma .PICHA NA WIZARA YA AFYA -DODOMA



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...