Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii

NAIBU Waziri wa Mfugo na Uvuvi atembelea shamba la AKM Glitters Company Ltd lililopo Dar es salaam eneo la Mbopo na Mbezi Beach, ambapo lengo la ziara yake ni kuangalia fursa walizonazo Watanzania katika ufugaji.

Akiwa katika ziara yake katika kampuni hiyo Naibu Waziri ulega ameona kazi mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo ikiwemo ya shamba la kuku wazazi, sehemu ya kutotoleshea vifaranga na chakula cha kuku wazazi.Ulega amesema ufugaji wa kuku ni fursa kubwa  ambayo ikiitumia vizuri, mhusika anaweza kuongeza kipato kwa mtu mmoja mmoja, na taifa zima kwa ujumla wake.

" Serikali lengo letu ni kuhakikisha nyama ya kuku isiwe kitoweo kwa watu wa juu tu, bali kiwe kwa hali zote kuanzia ngazi ya watu wa kipato cha chini na kati."Tunataka watu wote wajiingize kwenye ufugaji wa kuku, ili tuweze kujitosheleza wenyewe na tutoe ajira nyingi kwa watu ili kuendeleza tasnia hii ya kuku na kuuza kuku kwa bei ya chini kuliko kutegemea kuku kutoka nje,"amesema.

Amefafanua katika bajeti  ya serikali kwa mwaka huu wamependekeza pendekezo ambalo limeletwa Wizara ya Fedha na Mipango, kwamba riba imeondolewa kwa asilimia 5 kutoka kwa wakina mama na vijana."Sasa haitakuwa ni hiari kwa Halmashauri bali ni sheria kuwa Halmashauri zote kadri ya mapato yao ya ndani yanavyopatikana yatakwenda moja kwa moja kwa vijana na akina mama kwa asilima 5 kila mmoja," ameongeza.Amesema Serikali imeona hivyo, ili kusaidia hasa wakina mama walio wengi na kufuta riba hiyo.

Kwa upande wake Mkurugezi Mtendaji wa kampuni hiyo Elizabeth Swai alizungumzia suala la usafirishaji vifaranga ikiwa ni changamoto kuwafikia wakazi wa vijijini ambapo Naibu Waziri alisema, Serikali imejiweka katika mazingira mazuri katika hili kuhakikisha usafirishwaji unawafikia pia watu waliopo vijijini.
 Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiangalia kuku wa wazazi katika shamba la (AKM) lililopo Mbopo jijini Dar as Salaam.(picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wafanyakazi wa shamba la kuku wazazi,kituo cha kutotolea vifaranga mbopo jijini Dar as Salaam.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa shamba hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...