Na Agness Francis,Globu ya Jamii

WATANI wajadi Yanga Sc na SimbaSc wamepangwa kundi moja katika michuano ya Kombe la Kangame (CECAFA).

Simba na Yanga wamepangwa kundi C la michuano hiyo inayojumuisha timu 12 za Afrika Mashariki na Kati ambayo itaanza kutimua vumbi Juni 28 mpaka Julai 13 mwaka huu ambapo Tanzania watakuwa wenyeji wa michuano hiyo.Mashindano hayo yataonyeshwa kupitia Azam TV.

Michuano hiyo itachezwa nchini Tanzania kwa mitanange yake kupigwa kwenye Uwanja Mkuu wa Taifa (Tanzania Main Studium) na Uwanja wa Azam Chamazi Complex.

Akizungumza na vyombo vya habari leo katika hoteli ya Regency Jijini Dar es Salaam Rais wa shirikisho la mpira wa MiguuTanzania (TFF), Wallece Karia ametoa shukura kwa CECAFA pamoja na Azam kuleta tena mashindano hayo hapa nchini.

Karia amesema kuwa hiyo ni mara ya pili mfululizo kuwa wenyeji wa michuno hiyo ambapo ilifanyika kwa mara ya mwaka 2015 na matajiri wa Chamaz Azam Fc ndio walikuwa mabingwa wa kikombe hicho.

"Sisi tumepata tena fursa hii ya kuwa ndio wenyeji wa michuano hii iwe chachu kwa nchi zingine kuendeleza kufanyika kila mwaka bila kusimama"amesema Karia.

Katibu Mkuu Kagame Cup (CECAFA) Nicholas Musonye ameweka wazi timu zitakazoshiriki mashindano hayo kwa makundi ambapo mshida wa kwanza atajinyakulia kitita cha Dola za Marekani 30, 000, wa pili dola 20, 000 na wa tatu kupata dola 10,000.

"Kundi A ni Azam (Tanzania), Uganda Reps (Uganda),JKU (Zanzibar), KatorFC (Sudani Kusini ), ambapo kundi B ni Rayon (Rwanda),Gor Mahia (Kenya),Lydia Ludic (Burundi),ports (Djibouti) Huku kundi C ni Yanga (Tanzania),Simba (Tanzania),St.George (Ethiopia) na Dakadaha (Somalia)" amesema Musonye.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...