Na Zainab Nyamka, Globu ya jamii

KUELEKEA Mkutano mkuu wa Yanga Juni 10 mwaka huu, uongozi umeweka wazi ajenda kuu zitakazojadiliwa huku ajenda ya uchaguzi ikiwa imewekwa kando kwanza.

Maandalizi ya mkutano huo kwa wanachama wa Klabu ya Yanga yameshika kasi sasa zikiwa zimesalia siku nne kuelekea mkutano huo muhimu utakaotoa dira kwa klabu hiyo.

Akielezea masuala mbalimbali kuhusu maandalizi ya mkutano huo leo jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema wako hatua za mwisho kukamilisha maandalizi ya mkutano huo utakaofanyika kwenye ukumbi wa maofisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.

Mkwasa amesema wanakusudia kuwaalika watu mbalimbali akiwemo aliyekuwa Mwenyekiti na mfadhili wa klabu hiyo, Yusuph Manji.

"Tunatarajia kuwaalika watu mbalimbali akiwemo Yusuph Manji ambaye alikua mwenyekiti na mfadhili wa klabu hii, Baraza la Michezo,TFF  pamoja na wizara husika,"amesema Mkwasa.

Mwaliko utapelekwa pia kwa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Moja ya ajenda katika Mkutano huo maalumu kwa wanachama ni kujadili masuala mbalimbali ya klabu hiyo, ikiwa pamoja na suala zima la mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji.

Katika ajenda zingine zinazotarajiwa kuwasilishwa kwenye mkutano huo ni pamoja na kujadili ushiriki wa Yanga katika michuano ya kimataifa ikiwemo hatua waliyofika kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho, Mapato na Matumizi, bila ya kusahau Mabadiliko kuhusu mfumo wa uendeshaji.

Pia katika suala la uchaguzi wa kujaza nafasi zilizo wazi huenda litawasilishwa kupitia mengineyo.Hata hivyo kuna uwezekano mkubwa kwa ajenda hiyo kuondolewa ili kuwapa nafasi wanachama kujadili masuala muhimu.

Kwa upande wa Kaimu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga amesema mkutano huo utakuwa na lengo la kuwaeleza wanachama matatizo yanayoikabili timu yao, kuhusu uchaguzi wa kuziba nafasi zililizo wazi utatangazwa baadaye.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...