Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii.

Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Dimani Zanzibar, Abdallah Sharia Amer, na mwenzake Julai 12, wamepandishwa katika kizimba cha mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za utapeli. Mbunge Hugo anashtakiwa pamoja na Dr. Athumani Rajabu.

Akiwasomea hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Janet Magoho amedai mbele ya Hakimu Mkazi Hamisi Ally kuwa, washtakiwa wametenda kosa hilo la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kati ya Julai 17 na Septemba 29 mwaka jana ndani ya Jiji la Dar es Salaam

Imedaiwa, siku hiyo washtakiwa hao kwa pamoja na kwa kudanganya walijipatia kutoka kwa Dr. Abdi Hirsi Warsame kiasi cha milioni 55 kwa kumdanganya kuwa wangemsambazia vifaa tiba vya hospitality huku wakijua kwa siyo kweli.
Hata hivyo, washtakiwa wote  wamekana kutenda kosa hilo na wamerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo wametakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya sh. M. 27.5 kila mmoja.
Pia ametakiwa kuwasilisha fesha taslimu kiasi cha Sh. 27.5 au kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirisha hadi Julai 13 (kesho) kwa ajili ya dhamana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...