Na Agness Francis, Globu ya jamii

Azam fc yatamba kumgaragaza mnyama simba katika fainali za kuwania kombe  la kagame cup (cecafa).

Timu hizo zote mbili za kutoka hapa nchini ambazo zimefanikiwa kutinga fainali zitashuka dimbani kesho majira ya saa 12 jioni kuchoshana nguvu  katika uwanja wa taifa Jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya jana azamfc kumuondosha gor mahia ya nchini kenya  katika michuano hiyo  kwa kipigo cha  mabao 2-0, sasa wanakutana na wekundu wa msimbazi katika kumjua nani ataibuka kidedea wa kombe hilo.

Akizungumza leo jijini Dar es  salaam msemaji wa Azam FC Jaffary Iddi Maganga amesema  kuwa kikosi chao kimejipanga vizuri kuhakikisha wanatetea ubingwa  wao wa mwaka 2015 ambapo  michuano hiyo ilifanyika kwa mara ya mwisho hapa nchini. 

Jaffary amesema maandalizi waliyofanya ni mazuri na ndio maana wamefanya vema  na mpka kufikia hatua hiyo.

"Tunaiheshimu simba ni timu kongwe ya muda mrefu ilio na kikosi mahiri lakini sisi azam tunaliamini benchi letu la ufundi pamoja na mwalimu,tunaahidi kufanya vizuri  kwa kumfunga simba"amesema jaffary.

Mtanange huo utakaokuwa wa ina yake wa kiburudani kwa mashabiki ,inaonyesha zahiri kuwa soka la Tanzania limezidi kuimarika katika ukanda huu wa Afrika mashariki na kati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...