Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za utambulisho
kutoka kwa Balozi mteule wa Kenya hapa nchini Dan Kazungu Ikulu jijini Dar es
Salaam leo Julai 30, 2018
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika
mazungumzo Balozi mteule wa Kenya hapa nchini Dan Kazungu mara baada ya kuwasilisha Hati zake za
Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam leo Julai 30, 2018
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya Picha kutoka
kwa Balozi mteule wa Kenya hapa nchini Dan Kazungu. Zawadi hiyo ya picha
imetoka kwa Mama mzazi wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Mama Ngina Kenyatta na
katika picha hiyo anaonekana Rais Dkt. Magufuli akiwa na Rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta pamoja na Mama Ngina Kenya walipokuwa Nairobi nchini Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Balozi wa Kenya nchini Mhe. Dan Kazungu hati ya kiwanja cha kujengea mjini Dodoma kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2018
Balozi wa Kenya nchini Mhe. Dan Kazungu akielekea kuketi baada ya kupatiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli hati ya kiwanja cha kujengea mjini Dodoma kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2018. Hii ilikuwa kazi ya kwanza kwa balozi huyu ambaye alijiunga na wenzie baada ya kukabidhi hati za utambulisho kwa Rais muda mfupi uliopita.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...