Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe (MB), ametembelea na kuona miradi mbalimbali inayotekelezwa Mkoani Geita akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Mhandisi Robert Gabriel, Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Shaaban Ntarambe, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Mhandisi Deusdedith Kakoko, pamoja na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Geita Mhandisi Harun Senkuku. 

Miradi aliyoitembelea ni pamoja na Bandari ya Nyamirembe iliyoko kijiji na Kata ya Nyamirembe Wilayani Chato ambayo ilikua ikitumika tangu enzi ya Mkoloni ambayo kwa sasa haifanyi kazi. Waziri amewaeleza wananchi wajiandae kufurahi kwani muda si mrefu bandari hiyo itafufuliwa na kuanza kazi; ni baada ya kujitokeza kumlaki kwa fuaraha baada ya kumuona akitembea kwenye bandari hiyo. 

Amesema “mwezi wa nane mwaka huu tunasaini mkataba, tunairudisha Bandari ya Nyamirembe. Na sasa tunajenga meli kubwa, itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria elfu moja mia mbili (1,200), mizigo tani mia nne (400) ambayo itapita hapa kwenda Bukoba ndiyo maana kituo hiki lazima tukijenge na mkandarasi anaingia hapa mwezi wa nane. 

Hivyo ni ushindwe mwenyewe mwananchi kwa sababu sasa meli itakuwepo, barabara ya lami ipo, kiwanja cha ndege kinaendelea kujengwa unataka nini tena?” alimaliza kwa kushangiliwa na wananchi. 

Kisha,  Waziri ametembelea na kujionea maendeleo ya hatua ya ujenzi wa barabara ya Bwanga – Biharamulo yenye urefu wa kilomita sitini na saba (Km.67) inayojengwa kwa kiwango cha lami na kufurahishwa na hatua iliyofikiwa baada ya kupewa taarifa kuwa, barabara hiyo imeshajengwa hadi kilomita hamsini na saba (Km.57) hivyo bado kilometa kumi (Km.10) ili iweze kukamilika. 
 kibao cha bandari ya nyamirembe
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe (wa pili kushoto) na alioambatana nao wakitafakari jambo.
 Mkuu wa mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel (mweye kofia nyeusi-kulia) ,akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa mamlaka ya bandari,Mhandisi Deusdedith Kakoko, (kushoto) wakitembea wakati wa ukaguzi wa bandari hiyo.
Barabara ya bwanga-biharamulo
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe (kulia) akipeana mkono wa kwaheri na Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...