Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mchezaji wa zamani wa simba Juma Luizio amereja katika timu yake ya zamani Mtibwa Sugar ili kukitumia kikosi hicho cha Mabingwa wa Kombe la Azam Sports Federation (FA).

Mabingwa wa kombe la FA  leo wamefanikisha kuinasa saini ya Juma Luizio ambaye alitimka kwenda kucheza soka la kulipwa nchini Zambia katika Klabu ya Zesco kabla ya kuja kwa mkopo kwenye Klabu ya Simba.

Luizio aliyekuzwa na timu ya vijana ya Mtibwa Sugar  amekuwa na msimu mbaya katika klabu ya Simba akiwa hapati nafasi kwenye kikosi cha Mabingwa hao wa Ligi Kuu Ya Vodacom msimu wa 2016/17.

Kurejea kwa Luizio kwenye klabu ya Mtibwa yawezekana ameenda kuziba nafasi ya Hassan Dilunga anayewaniwa na klabu ya Simba na kukiwa na uhakika wa tayari ya kumwaga wino kwa wekundu hao wa msimbazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...