Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

Benki ya Credit Suisse ya nchini Uingereza imeonesha nia ya kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa zaidi ya Dola milioni 200 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo miradi mikubwa ya Nishati ya Umeme na miundombinu ya Reli.

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es Salaam katika Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Ujumbe wa Benki ya Credit Suisse ya Uingereza ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo Bw. Lawrence B. Fletcher, kuhusu ushirikiano katika miradi ya maendeleo.

Dkt. Mpango alisema kuwa tayari zipo hatua mbalimbalimbali zimefikiwa katika kufanikisha upatikanaji wa Mkopo kutoka Benki ya Suisse hivyo kuwa na tumaini la kupata kiasi cha Dola milioni 200 katika mwaka wa fedha wa 2018/19 .

“Miradi ya Kipaumbele ambayo Serikali inaitekeleza ni pamoja na Ujenzi wa Reli kwa kiwango cha Kimataifa (SGR), kufufua Shirika la Ndege Tanzania kwa kununua Ndege mpya na miradi ya umeme ambayo itachochea maendeleo ya watu na Taifa kwa ujumla”, alieleza Dkt. Mpango.

Aliitaja miradi mingine ambayo Serikali ina mpango wa kuitekeleza kuwa ni pamoja na Ujenzi wa Bwawa la Umeme la Rufiji (Rufiji Haydro Project) ambalo kukamilika kwake kutasaidia kuzalisha umeme wa Megawati 2100 ambao utatumika katika kuchochea uchumi wa viwanda unaohitaji umeme wakutosha.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango akipokea picha ya alama ya ushirikiano ya kiasi cha Dola 500 kutoka kwa Afisa mwandamizi wa Benki ya Suisse ya Uingereza Bi. Elizabeth Muchemi, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Mchumi Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Omary Khama (kulia), anayeshughulika na maswala ya uchambuzi wa madeni akimwelezea Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia) kuhusu miradi mbalimbali itakayotekelezwa kutokana na pesa iliyopatikana, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Benki ya CREDIT SUISSE.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (kulia) akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wea Benki ya Suisse Bw. Lawrence B. Fletcher kwa mikopo mbalimbali ambayo Benki hiyo imetoa kwa Serikali ya Tanzania katika Sekta mbalimbali, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...