THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

CCM YAKABIDHI GARI LA KUBEBA WAGONJWA KWA WANANCHI LENG'ATA

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimekabidhi gari la kubeba wagonjwa katika Kata ya Leng'ata wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.

Kukabidhiwa kwa gari hiyo ni moja ya mkakati wa CCM wa kuendelea kutekeleza ahadi ya kuboresha na kusogeza huduam za afya karibu na wananchi kwa kufanikisha kupatikana kwa gari hiyo.

Gari hiyo imekebidhiwa jana katika kituo cha afya cha Kagongo ambapo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole ndio aliyekabidhi kwa niaba ya Rais John Magufuli ambaye ndiye aliyetoa gari hilo baada ya kupokea kilio cha wananchi kupitia Mbunge wa Jimbo la Mwanga Proesa Jumanne Maghembe

Akizungumza baada ya kukabidhi gari Polepole amesema Rais Magufuli anawapenda wananchi wote bila kubagua vyama vyao."Na CCM nayo inahimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 mpaka 2020 hata katika maeneo yanayoongozwa na upinzani ndio maana gari la kubebea wagonjwa limetolewa katika Kata yenye Diwani wa upinzani ili kuendeleza dhana ya CCM kuwa maendeleo yanayotolewa na Serikali ya CCM hayana chama,"amesema.