Na Frankius Cleophace, Tarime

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo( Chadema)Kata ya Sirari wilayani Tarime mkoani Mara kimemvua uongozi na kumfutia uanachama aliyekuwa Mwenezi wa kata hiyo Samwel Kijiji Mwita kutokana na tuhuma za upotevu wa fedha Sh.80,000 zilizochangwa kwa ajili ya kununua jeneza katika msiba wa aliyekuwamwanachama wa chama hicho marehemu Chacha Makuri.

Mwita Isansi ni Mwenyekiti wa Chadema Kata ya Sirari amesema wameamua kumfutia uanachama Mwita kutokana na tuhuma hizo za upotevu wa fedha.Mwita amesema kuwa zilichangwa ni Sh.320,000 kwa lengo la kununu jeneza nchini Kenya lakini baadae zilipungua Sh.80,000.

“Baada ya upotevu wa fedha hizo sisi kama viongozi tulijichanga ili kununua jeneza baada ya msiba tumemuita kamati ya maadili takribani mara mbili lakini hajaweza kuitikia na maamuzi yetu ni kumfuta uanachama na kumvua uongozi kwahiyo mpaka sasa siyo kiongozi,” amesema Mwita.

Mwenyekiti huyo ametoa mwito kwa viongozi wengine kuendelea kuzingatia maadili ya uongozi na sikufanya ubadhilifu wowote na kusema kuwa chama kitaendelea kuchukua hatua kali kwa viongozi ambao wanaenda kinyume na maadili ya uongozi.

Aidha Mwenyekiti wa kijiji cha Sokoni Denson Makanya amesema kuwa licha ya kutafuna fedha hizo bado Mwenezi huyo amekuwa akituhumiwa kwa makosa mbalimbali na tayari alishaandikiwa barua ya onyo juu ya vitendo vyake alivyokuwa akifanya akiwa kiongozi ndani ya jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...