*Ni ya mwamvuli unaotumia mionzi ya jua kutengeneza umeme, kuanza kutumika Karagwe

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
CHAMA cha Kukuza Uhusiano kati za Tanzania na China umefanikisha kupatika kwa msaada wa miavuli 100 inayotumia nguvu ya jua kuzalisha umeme ambayo imekabidhiwa kwa Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.

Miavuli hiyo ambayo ni teknolojia mpya iliyozinduliwa China inakwenda kuanza kutumika wilayani humo kwenye baadhi ya shule, zahanati na kituo cha afya kwa lengo la kuhakikisha nishati ya umeme inapatikana kwa ustawi wa maendeleo ya nchi yetu.

Msaada huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Taasisi ya Maendeleo ambayo ipo chini ya Chama cha Kikomunisti cha China(CPC).

Hivyo Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa wa CPC Song Tao ndio aliyokabidhi msaada huo ambapo amesema wanatambua urafiki , udugu na ujamaa wa nchi hizo mbili na hivyo wanatambua umuhimu wa kuendelea kuisaidia Tanzania.

Akizungumzia msaada huo Katibu Mkuu wa Chama cha Kukuza Uhusiano wa Tanzania na China Joseph Kahama amesema msaada huo umetokana na jitihadaza chama chao katika kuhakikisha uhusiano wa nchi hizo mbili unaendelea.

Amefafanua kuwa Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kuzinduliwa kwa teknolojia hiyo ambayo kwa hapa nchini itakwenda kuanza kutumika wilayani Karagwe.

Amesema miavuli hiyo ya jua itasaidia kuweka mazingira mazuri ya wanafunzi kusoma katika shule ambazo msaada utapelekwa na kufafanua kuwa giza litakapoingia basi wafunzi watapata mwanga kupitia msaada huo.

Pia amesema kwenye vituo vya afya na zahanati  msaada huo unakwenda kusaidia kuboresha mazingira ya utoaji huduma za afya na kueleza miavuli hiyo inaweza kutumika katika vifaa mbalimbali vinavyotumia umeme.

"China imeamua kuitumia Tanzania kuzindua teknolojia hiyo ambayo haiko mahali kokote duniani .Tumepewa miavuli 100 na mingine itaingia nchini Oktoba mwaka huu .

Alipoulizwa kuhusu thamani ya msaada huo amejibu kuwa hawezi kuifahamu ila anachojia teknolojia mpya nayo ina gharama zake.

Awali Mwenyekiti wa Chama cha Kukuza Uhusiano wa Tanzania na China Dk.Salim Ahmed Salim ameipongeza nchi ya China kwa msaada huo na ni uthibitisha unaodhihirisha urafiki wao wa muda mrefu.



KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...