Na Said Mwishehe,Globu ya jamii.

CHUO cha Maji kimesema changamoto kubwa iliyopo katika sekta ya maji nchini ni uhaba wa watalaamu ,hivyo jukumu la chuo hicho kuendelea kuandaa watalaamu  ambao watakuwa watakuwa wamebobea katika eneo sekta ya maji ili kuondoa changamoto hiyo.

Katika kuhakikisha changamoto hiyo inamalizwa Chuo hicho kimetoa rai kwa Watanzania na hasa vijana ambao wamesoma masomo ya sayansi na kufaulu vizuri wakajiunga na chuo hicho kwani tayari wameanza kupokea maombi ya wanaotaka kujiunga na chuo hicho kwa mwaka wa masomo unaonza 2018.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam katika Maonyesho ya 13 ya Vyuo Vikuu ya Elimu ya Juu Tanzania (TCU) na Ofisa Masoko wa Chuo cha Maji Ghanima Chanzi.Amesema kuwa chuo hicho kimedhamiria kuondoa changamoto hiyo kuwa kuhakikisha wanapatikana wahitimu waliohitimu masomo yanayotolewa na chuo hicho kwa ajili ya kulitumikia taifa kaika eneo la sekta ya maji.

"Wapo watalaam ambao wanatoa huduma katika eneo hilo lakini bado kuna changamoto kubwa , hivyo jukumu letu ni kuwapika watalaam ambao ndio wenye kujua vema eneo la maji."Hivyo kadri ambavyo wahitimu wataendelea kumaliza chuoni hapo watakwenda kuondoa changamoto maana tutakuwa tunaongeza watalaam mwaka hadi mwaka.Hivyo kikubwa tunaomba Watanzania kujiunga kwenye chuo chetu  ili waje kuwa wahandisi wa maji,"amesema.

Hivyo amesisitiza wanafunzi wasome masomo ya sayansi ili wawe wataalam wa maji na kufafanua wameanza kupokea maombi kupitia tovuti ya www.waterinstitute.ac.tz.Amefafanua wanafunzi wanaosoma masuala ya maji katika chuo cha maji wengi wao wanapata ajira kwani wanahitajika zaidi na kueleza waliohitimu mwaka jana hakuna ambaye amebaki mtaani.

Kuhusu mafunzo yanayotolewa chuoni hapo amesema yapo katika ngazi ya Stashahada na Shahada na baadhi ya kozi zinazotolewa ni Uhandisi wa usambazaji maji na usafi wa mazingira,Uhandisi na umwagiliaji, Ubora wa maji (maabara),Maji na hali ya hewa na Uchimbaji visima.

Moja wa Maofisa wa chuo cha maji akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea katika banda lao katika maonesho ya vyuo vikuu yanayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...