Na Leandra Gabriel, Blogu jamii
CHUO cha Ustawi wa Jamii kilichopo Kijitonyama jijini Dar es salaam kimeanza kudahili wanafunzi kwa mwaka 2018/2019  katika maonesho al maarufu kama maonesho ya TCU yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi mmoja.

Akizungumza na Michuzi blog Msajili wa Chuo hicho Nuru Kalufya ameeleza kuwa katika kupokea wanafunzi katika msimu huu na wanasajili kupitia mtandao (online) bure na kinachohitajika ni wanafunzi kuwa na vyeti vyao na namba zao za usajili (index number) na watapata huduma hiyo ya udahili na ushauri wa kitaaluma bure kabisa.

Kuhusu kozi zinazotolewa na Chuo hicho bi. Nuru ameeleza kuwa wanatoa kozi tano kwa gharama nafuu kabisa na hii ni kuanzaia ngazi ya cheti, stashahada, shahada, uzamili na post graduate ya kozi ya Health System Management ambayo ni mpya kabisa chuoni hapo.

Akizungumzia kuhusiana na usajili wa Chuo Nuru amesema kuwa wamesajili na wanatambulika na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) pamoja na NACTE na Serikali kwa ujumla.Hivyo wazazi na  wadahiliwa wasiwe na hofu.

Aidha ameeleza kuwa watatoa huduma katika maonesho hayo hadi kesho majira na saa kumi na moja jioni na baadaye wataendelea kutoa huduma hizo katika chuo chao kinachopatika Kijitonyama hivyo wanafunzi waendelee kujitokeza kwa wingi zaidi.

Kwa upande wake Mshauri wa wanafunzi bi. Silvia Ngiga amewahakikishia wanafunzi usalama pindi wawapo shuleni na wanafunzi watokao mikoani watapata za malazi  na huduma nyingine za kijamii ni za kuaminika katika chuo hicho.
Msajili wa Chuo cha ustawi wa jamii Nuru Kalufya akizungumza na blogu ya jamii kuhusu mikakati walioweka katika kudahili wanafunzi wapya 2018/2019
 Mshauri wa wanafunzi wa chuo cha Ustawi wa jamii Silvia Ngiga akizungumza na Michuzi blog kuhusiana na maonesho katika maonesho  ya TCU yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi mmoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...