Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

TUME ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) imesema kuwa barua iliyokuwa katika mitandao ya jamii ni yao isipokuwa wanasikitishwa kuiona katika mitandao hiyo kabla haijajibiwa na wahusika wa barua hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Costech Dk.Amos Nungu (pichani) amesema lengo la barua hiyo ilitakiwa kujibiwa na sio kusambaa katika mitandao ya jamii.

Amesema kazi ya Tume ni kuishauri Serikali katika masuala yote ya Sayansi na teknolojia na ubunifu na kuandaa vipaumbele vya utafiti pamoja na kupanga mgawanyo wa matumizi ya rasilimali wanazopewa na Serikali.

Amesema kazi zingine za tume ni kuratibu kufanya tathimini na ufatiliaji wa tafiti na uendelezaji wa Teknolojia.

Ameongeza tume inayo kamati maalumu inayohusika na utoaji wa vibali kwa tafiti mbalimbali zinazoendeshwa hapa nchini.
"Tunasikitika kuona barua tulioitoa kwa TWAWEZA inasambaa mtandaoni wakati hata majibu hajapatikana kwa wahusika,"amesema Dk.Nungu.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...