Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ally Hapi akiwa ameambatana na wakuu wa idara mbalimbali kutoka ofisini kwake  mapema jana ameanza ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ya Wananchi na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili Wananchi wa Wilaya hiyo.

Katika ziara hiyo iliyoanza jana kata ya Tandale Mkuu huyo wa Wilaya ameweza kusikiliza kero za wananchi waishio maeneo hayo,katika utangulizi wake alisema ni jukumu lake kuwasikiliza na kuzitatua kwani ndiyo jukumu ambalo Rais kamuagiza kulifanya."Nimejipanga na timu yangu kuanza ziara yangu na nitazunguka kata hadi kata kuwatembelea wananchi na kusikiliza kero zinazowakabili wananchi wangu, hiyo ndo kazi nimepewa kama mkuu wenu wa wilaya.

Serikali ya awamu ya tano inafanya mambo mengi sana na kwa sababu serikali ni kubwa inawezekana sisi tukikaa juu tusijue yanayoendelea huku chini vizuri, wapo wananchi wanaoteseka kwa kukosa haki zao, wananchi ambao wananyanyasika, wananchi wenye kero mbalimbali zinazohusu maji, afya, elimu, ardhi, jeshi la polisi na n.k. Kwasababu mimi sio mtu wa kukaa ofisini nimeamua kuanzaisha huu mchamchaka kata hadi kata kuwasikiliza Wananchi" DC Hapi

Katika ziara hiyo wananchi waliibua kero zao mbalimbali zikiwemo huduma mbovu katika Zahanati ya Tandale, ukosekanaji wa dawa katika Zahanati hiyo, migogoro ya ardhi, tatizo la maji, wazee kutopata fedha zao stahiki na kupewa watu wanaojiweza, migogoro ya mirathi, shutuma za polisi jamii kuwapiga wananchi kinyume na sheria, ujenzi wa barabara, ujenzi wa shule ya sekondari katika kata hiyo na kadhalika.

Aidha DC Ally Hapi ametoa maagizo kwa wakuu wa idara husika kushughulikia kero hizo za wananchi za kuhakikisha zimepatiwa ufumbuzi wa kina ili wananchi wa kata hiyo wasiendelee kuteseka na kujivunia nchi yao.Katika hali nyingine Wananchi wa maeneo hayo walionekana kufurahishwa na ziara ya mkuu huyo wa wilaya kwani walikua wanatamani sana kukutana nae ili waeleze kero zao mbele yake lakini ikawa inawapa ugumu hivyo wamemshukuru.

DC Hapi atafanya ziara ya kuzunguka na kusikiliza kero za wananchi kwenye kata zote 20 Za Wilaya ya Kinondoni na Kwa Siku Ya Kesho Jumanne Atakua Kata Ya Kinondoni Uwanja Wa Ufipa Kipande.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ally Hapi akiwa ameambatana na wakuu wa Idara mbalimbali kutoka ofisini kwake mapema jana wakati akiendelea na ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya Wananchi na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili Wananchi wa Wilaya hiyo. 
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ally Hapi akiwa akiwahutubbia wakazi wa Tandale mapema jana wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya Wananchi na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili Wananchi wa Wilaya hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...