Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Idd Hassan Kimanta Jumatano Julai 11, 2018 amezindua kiwanda kidogo cha kuchakata Ngozi na kutengeneza bidhaa za ngozi kiwanda hicho kipo katika kijiji cha Mswakini na kutoa vyeti kwa wanakikundi waliofuzu mafunzo.
Kiwanda hicho ni matokeo ya kikundi cha akinamama 22 ambao mwezi Agosti 2017 walijiunga pamoja na kupata ufadhili kutoka shirikikala OIKOS kwa lengo kujijenga kiuchumi kupitia Ngozi na kuunga mkono Juhudi za Serikaliya kuelekea Tanzania ya Viwanda.
Katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya huyo amewapongeza akinamama hao kwa uamuzi wao huo na kuwaahidi kuwa  kupitia halmashauri ya wilaya ya  Monduli atahakikisha wanapata Mkopo ili kuongeza mtaji.
Pia amelishukuru Shirika la Misaada la Marekani-USAID kwa kulipatia fedha shirika la OIKOS ambalo ndilo lililosimamia mchakato wote kupitia Mradi wa Ikolojia Hatarini Kaskazini mwa Tanzania.
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe.Idd Hassan Kimanta  akikata utepe kuashiria uzinduzi kiwanda cha kuchakata bidhaa za ngozi zinazotengenezwa na kiwanda kidogo cha kuchakata Ngozi kilichopo katika kijiji cha Mswakini,wilayani Monduli
 Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe.Idd Hassan Kimanta  (pichani kati) akitazama baadhi ya bidhaa za ngozi zinazotengenezwa na kiwanda kidogo cha kuchakata Ngozi kilichopo katika kijiji cha Mswakini,wilayani humo.
 Mkuu wa Wilaya ya Monduli,Idd Hassan Kimanta akitoa vyeti kwa baadhi ya Wanakikundi waliofuzu mafunzo.
 Baadhi ya Bidhaa za ngozi zikiwa tayari kwa kuuzwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...