Na Jacquiline Mrisho -  MAELEZO
Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) imejipanga kuanza kutoa mafunzo endelevu ya matumizi ya kemikali katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ili kuongeza uelewa wa matumizi bora ya kemikali hizo.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko alipokuwa akifunga mafunzo ya siku tatu juu ya matumizi ya kemikali kwa jumla ya wanafunzi 40 wa Chuo Kikuu cha Dodoma wanaosoma masomo ya Uhandisi wa Uchenjuaji Madini.

Dkt. Fidelice amesema kuwa moja ya kazi za Mamlaka hiyo ni kutoa elimu kwa wadau wa kemikali ili kuwawezesha kufahamu matumizi bora ya kemikali yakiwemo ya uzalishaji, usafirishaji, uuzaji pamoja na uhifadhi wa kemikali.

"Mafunzo ya masuala ya kemikali ni ya muhimu hasa ukizingatia nchi yetu inaelekea katika uchumi wa viwanda ambapo matumizi ya kemikali yataongezeka hivyo tunajipanga kuweka mikakati bora ambayo itatuwezesha kutoa mafunzo ya kemikali chuoni hapa kwa wanafunzi wanaosoma kozi zinazohusisha matumizi ya kemikali", alisema Dkt. Mafumiko.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyesimama) akitoa hotuba wakati wa kufunga mafunzo ya siku tatu ya Usimamizi Salama wa Kemikali kwa wahitimu wa masomo ya Shahada ya Uhandisi wa Sayansi ya Madini na Uchakataji Madini (B.Sc. Metallurgy and Minerals Processing Engineering) wa Chuo cha Sayansi ya Ardhi (CoES), Chuo Kikuu cha Dodoma, yaliyofanyika mkoani Dodoma.
Mkuu wa Chuo cha Sayansi ya Ardhi (CoES), Chuo Kikuu cha Dodoma, Profesa William Mwegoha (aliyesimama), akizungumza kabla ya Mgeni Rasmi wakati wa kufunga mafunzo ya siku tatu kuhusu Usimamizi Salama wa Kemikali kwa wahitimu wa masomo ya Shahada ya Uhandisi wa Sayansi ya Madini na Uchakataji Madini (B.Sc. Metallurgy and Minerals Processing Engineering) yaliyofanyika Dodoma na kuandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Kati, Mkoani Dodoma.
 Washiriki wa mafunzo ya Matumizi Salama ya Kemikali yaliyotolewa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Kati, wakifuatilia hotuba ya kufunga mafunzo hayo iliyokuwa inatolewa na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (hayupo pichani).
Kaimu Meneja wa Maabara ya Kanda ya Kati, Bw. Musa Kuzumila, akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Usimamizi Salama wa Kemikali kwa wahitimu wa masomo ya Shahada ya Uhandisi wa Sayansi ya Madini na Uchakataji Madini wa Chuo kikuu cha Dodoma.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo mmoja wa washiriki wa mafunzo ya Usimamizi Salama wa Kemikali.
 Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, akiwa pamoja na Mkuu wa Chuo cha Sayansi ya Ardhi (UDOM), Prof. William Mwegoha, watumishi wa Chuo, watumishi wa Maabara ya Kanda ya Kati na wahitimu walioshiriki mafunzo ya Usimamizi Salama wa Kemikali mara baada ya kufunga mafunzo hayo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...