Na Mathias Canal-WK, Bukoba-Kagera

Malalamiko ya muda mrefu ya wakulima yaliyokuwepo kwamba ushirika unatoa bei ndogo, sasa yamepatiwa muarobaini baada ya serikali kupitia kwa kina gharama za uendeshaji na uongezaji thamani kwa zao la kahawa kwa Vyama vikuu vya ushirika Mkoani Kagera.

Serikali imepiga marufuku kwa vyama hivyo vya ushirika kutoza zaidi ya shilingi 490 kwa kilo moja ya Kahawa ya maganda kama gharama za uendeshaji na uongezaji thamani, Awali maainisho ya gharama hizo yalikuwa ni makubwa ambapo kiasi cha shilingi 1350 kwa kilo moja ya Kahawa ya maganda ilianishwa kama gharama za uendeshaji.

Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba ameeleza agizo hilo Leo 12 Julai 2018 wakati akizungumza na wajumbe wa Halmshauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera kwenye Hoteli ya Bukoba Coop ambapo miongoni mwa ajenda ya kikao hicho ilikuwa ni kujadili kuhusu soko la Kahawa na uendeshaji wa ushirika.

Dkt Tizeba amewaeleza wajumbe hao kuwa amepiga marufuku hiyo kufuatia malalamiko ya wadau wa Kahawa Mkoani Kagera ambapo gharama hizo zilionekana kuwa kubwa ukilinganisha na gharama halisi.

"Ndugu zangu wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM inawezekanaje shilingi mia mbili inatozwa kama ushuru wa chama kikuu, na shilingi mia mbili tena inatozwa kama ushuru wa chama cha msingi, ni nani anaweza kukupa faida namna hii sasa rasmi ushuru huu tumeupunguza kama nilivyoeleza" Alikaririwa Mhe Tizeba
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akitoa ufafanuzi kuhusu sintofahamu ya biashara ya kahawa wakati akizungumza kwenye mualiko maalumu na wajumbe wa Halmshauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera kwenye Hoteli ya Bukoba Coop, Leo 12 Julai 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Wajumbe wa Halmshauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wakisikiliza ufafanuzi wa Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba kuhusu sintofahamu ya biashara ya kahawa wakati akizungumza kwenye mualiko maalumu na wajumbe wa Halmshauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa kwenye Hoteli ya Bukoba Coop, Leo 12 Julai 2018.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera Bi Costansia Buhiye akitoa neno kwa niaba wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Mkoani humo mbele ya Waziri Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba kutokana na ufafanuzi alioutoa kuhusu sintofahamu ya biashara ya kahawa wakati akizungumza kwenye mualiko maalumu na wajumbe wa Halmshauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera kwenye Hoteli ya Bukoba Coop, Leo 12 Julai 2018.
Waziri Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akijadili jambo na Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Kagera Mhe Oliver Semuguruka mara baada ya kutoa ufafanuzi kuhusu sintofahamu ya biashara ya kahawa wakati akizungumza kwenye mualiko maalumu na wajumbe wa Halmshauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera kwenye Hoteli ya Bukoba Coop, Leo 12 Julai 2018.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...