Baada ya kukamilika kwa maonyesho ya vuo Vikuu, Kampuni ya Global Education Link, imetangaza kuanza kwa Maonyesho ya Global Education Link yanayohusisha vyuo vya nje, yanayoanza Jumapili ya Kesho, 20/07/2018 yatakayofanyika katika ukumbi wa Makao Makuu ya Global Education Link, yaliyopo eneo la Chang'ombe, kwenye kituo cha Mafuta cha Oicom kwenye kona ya kuelekea Veta Chang'ombe.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link, Abdulmalik Mollel, baada ya kukamilika kwa maonyesho ya vyuo vikuu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu, CTU yaliyomalizika leo..
Bwana Mollel amesema, Global Education Link, imeamua kufanya maonyesho hayo, kufuatia kuanza kwa utaratibu wa mikopo kwa wanafunzi wanaotaka kusoma vyuo vikuu vya nje ya nchi, kulikopelekea wanafunzi kujitokeza kwa vingi kutafuta vyuo vya nje.

Katika kulitimiza hili, wawakilishi kutoka vyuo vikuu 10 vya nje ya nchi, tayari wameishatua nchini kwa ajili ya maonyesho hayo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...