Ikiwa miongoni mwa makampuni ya simu yanayofanya vizuri kwa sasa barani Afrika.  Infinix inaendelea kuchomoza kimatafaifa baada ya kuzindua Infinix NOTE5 simu iliyobeba sifa zote kubwa zenye kumfanya mtumiaji wa simu janja kutoifumbia macho. toleo hili limefuatia baada ya mafanikio ya Infinix NOTE 4.

Infinix NOTE 5 ni simu ya kwanza kuzalishwa na kampuni ya Infinix inayotumia mfumo wa Android One na kupewa ujazo mkubwa wa betri ya 4500mAh lakini pia Infinix NOTE 5 inatumia processor aina ya Helio P23 ya 2.0 Ghz Octor core ambapo sifa zote hizo zimeifanya simu ya Infinix NOTE 5 kuwa na uwezo wa kukaa na chaji siku tatu na zaidi pasipo masharti katika utumiaji.
Pamoja ya kuwa na betri lenye ujazo mkubwa lakini pia ili kuepuka upotezefu wa muda Infinix NOTE 5 inatumia mfumo wa first chaji wenye kujaza simu kwa haraka.

Na kutokana na sifa ya Android One, betri ya 4500mAh, processor ya 2.0 Ghz Octor core na chaji yenye kujaza simu kwa haraka zinaifanya Infinix NOTE 5 kuwa simu halali hasa kwa wale watu wa maofisini, wasafiri lakini na hata kwa wale wanaoshinda mitandaoni, wapenzi wa movies na games.

Ni simu ambayo inaweza wapendeza wapenda kamera kutokana na namba za pixel ya kamera ya nyuma kuwa  kubwa ikiwa na 12MP na 1.25um na 16MP iliyo na low light selfie na kamera zote zikiwa na aperture kubwa ya 2.0 yenye kuruhusu mwanga kupenya katika  kamera wakati wa upigaji picha. Infinix NOTE 5 inakupa picha yenye uhalisia hata katika mwanga hafifu na hii ni kutokana na kamera zake kuwa flashi na pamoja ya kioo cha simu  chenye FHD (1080*2160).
Sifa nyengine
Wembamba wa simu 8.4mm
memory 32GB + 3GB
kamera 12 MP AF, F 2.0, 1.25um
processor 2.0 Ghz octor core
betri 4500mAh
kioo 6.0 FHD, 18:9
network 4G
Kwa habari nyingi zaidi tembelea tovuti www.infinixmobility.com/tz/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...