Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii

Upande wa mashtaka katika kesi ya mauaji inayomkabili mke wa bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita (41), umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa jalada la kesi lipo mikononi kwa  kwa mkurugenzi wa mashtaka (DPP).

Wakili mwandamizi wa Serikali, Patrick Mwita ameeleza hayo leo Jumatatu Julai 23, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakati shauri hilo lilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Mbali na Mrita, mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ya mauaji namba 5 ya mwaka 2017 ni mfanyabiashara Revocatus Muyela (40)  ambapo wote wanakabiliwa na shtaka mmoja la mauaji ya dada yake Erasto Msuya, Aneth Msuya.

"Shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa na jalada la kesi kwa sasa lipo mikononi mwa DPP bado tunalifuatilia "amedai Mwita.

Kufuatia taarifa hiyo, Hakimu Simba amewataka upande wa mashtaka kulifuatilia jalada hilo ambalo mwanzoni walidai liko ofisini kwa DPP na sasa liko mikononi mwake.

Wakili wa utetezi Peter Kibatala alikubaliana na upande wa mashtaka na kuiomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine fupi.

 Hakimu Simba ameahirisha  kesi hiyo hadi Julai 30, 2018 itakapotajwa tena.

Februari 23, 2017, washitakiwa hao waliachiwa huru na mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa na kisha wakakamatwa tena na baadaye kusomewa upya shtaka moja la mauaji.

Washtakiwa wanadaiwa kumuua kwa makusudi Aneth tukio linalodaiwa kutokea Mei 25, 2016 maeneo ya Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...