*Pia agusia aina ya suti anazovaa ambazo zimeibua mjadala

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola amesema kuwa kasi aliyoanza ndio ambayo itaendelea zaidi ya hapo na kusisitiza kasi yake ni kama gari imeanza na zero na sasa inazidi kwenda mbele.

Kuhusu kuona kuwa anavaa vazi la aina moja(Suti)kila siku amesema anazo nyingi lakini ameamua zote zinafanane , hivyo hata anapobadilisha hakuna anayejua.

Waziri Lugola ametoa kauli hiyo wakati anazungumza na Michuzi Blog kwa njia ya simu ambayo ilitaka kufahamu mambo mawili kutoka kwake likiwemo la mavazi anayovaa ambayo yamekuwa gumzo pamoja na kasi aliyoanza nayo.

Lugola ameteuliwa na Rais Dk.John Magufuli kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi baada ya kuondolewa kwa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Dk.Mwigulu Nchemba.

Hata hivyo baada ya kuteuliwa kwenye nafasi hiyo Lugola ameonekana kuwa na kasi kubwa katika kutekeleza majukumu yake.

Kuhusu mavazi Lugola amesema kuwa anazo nguo nyingi tu lakini amemua ziwe katika muonekano huo ambao sasa wengi wanauona na ataendelea kuonekana hivyo hivyo.

Wakati alipoulizwa hukusu kasi yake amesema "Kasi yangu ni kama vile unavyoona spidi ya gari ambayo inaanza na Zero lakini kadri unavyokanyaga mafuta ndivyo inavyoongezeka.

"Hivyo kasi ambayo nimeanza nayo ni kama Zero kwenye gari na itaongezeka zaidi ya hapo.Wanaodhani natania au nafanya mzaha wafahamu tu si tanii na wala sifanyi mchezo bali ninatekeleza majukumu yangu kwa kasi,"amesema Lugola.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...