*Ni baada ya gari ya kubeba mahabusu kuharibika

Na Dixon Busagaga, Moshi

KESI ya tuhuma za mauaji ya kukusudia linalomkabili mmilikiwa wa Shule ya Sekondari ya Scolastica Edward Shayo na wenzake wawili limehairishwa kwa mara ya tatu sasa na sababu ya kuahirishwa ikitajwa imetokana na kuharibika kwa gari la kubebea mahabusu.

Kwa jana kesi hiyo ilipangwa kuendelea kwa hatua ya usomaji wa maelezo ya mashahidi kwa ajili ya kufunga ushahidi kabla ya shauri hilo kuhamishiwa Mahakama Kuu. Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Sophia Masati alieleza kuwa shauri hiyo itatajwa kwa ajili ya usomaji wa maelezo ya mashahidi Agosti 3,mwaka huu.

“Kesi hii imeahirishwa hadi Agosti 3 mwaka huu kwa ajili ya kuja kusoma maelezo ya mashahidi wa kesi hii,"amesema Hakimu huyo.Kabla ya kutajwa kwa mara nyingine kwa shauri jana, Julai 6 mwaka huu Hakimu mkazi wa mahakama ya hakimi mkazi ,Moshi ,Julieth Mawole aliieleza maelezo ya ushahidi wa shauri hilo utatolewa .

Kwa mara ya kwanza usomaji wa maelezo ya kufunga ushahidi uliahirishwa baada ya washtakiwa kushindwa kufikishwa mahakamani.Sababu za kutofika kwa washtakiwa mahakamani hapo zilitajwa kuwa ni mkanganyiko wa tarehe iliyopangwa na mahakama hiyo ambayo ilikua ni June 29 mwaka huu kutofautiana na ile iliyowasilishwa Mahabausu Gereza la Karanga ambayo ilitajwa kuwa ni Julai 29 ,mwaka huu.

Maelezo hayo yaliwasilishwa mahakamani hapo na Wakili wa Serikali,Agatha Pima alipoomba kupangwa kwa tarehe nyingine kwa ajili ya kuendelea kwa hatua ya Kufunga Ushahidi kwenda Mahakama kuu.Ombi hilo lilipingwa na Wakili wa upande wa utetezi anaye mtetea Mshtakiwa wa Pili katika shauri hilo ,Edward Shayo,Elikunda Kipoko akieleza kutoridhishwa na maelezo ya upande wa Jamhuri .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...