Na Editha Karlo,blog ya jamii,Kigoma

MKOA wa Kigoma wapiga hatua Katika kuwezesha wananchi wake kiuchumi

mkakati ulioanzishwa na Serikali wa kuwainua wananchi kiuchumi na kuboresha maisha ya wananchi kwa ujumla, umeonekana kuzaa matunda makubwa katika Mkoa wa Kigoma kwa kuinua pato la uchumi kibiashara na shuguli za ujasiliamali kwa wanaume, wanawake na vijana.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brig. Jen. Mstaafu Emanuel Maganga ameyasema hayo leo wakati akikabidhiwa kombe na cheti cha ushindi kwa nafasi ya pili Kitaifa Katika kuwezesha wananchi kiuchumi katika ukumbi wa utamaduni Wilayani Kasulu.Maganga alisema kuwa juhudi kubwa ambazo zimefanywa na Serikali ya Mkoa wa Kigoma ni kusimamia na kuwawezesha wananchi kiuchumi ikiwa pamoja na kutoa mikopo, kuwapa elimu na mafunzo ya Ujasiliamali wanachi kupita Mabaraza ya Biashara ya Wilaya.

Afisa wa Dawati la Uwezeshaji Kiuchumi la Mkoa wa Kigoma (RECO) Deogratias Sangu ameeleza mafanikio ya kushika nafasi ya pili yametokana na kukidhi vigezo Katika utekelezaji wa mambo yote yaliyopangwa kama msingi wa kuinua wananchi kiuchumi.Sangu ameongeza kwa kusema kuwa Mwaka jana (2017) Mkoa wa Kigoma ulishika nafasi ya mshindi wa tatu Kitaifa, na kwamba juhudi kubwa imefanyika katika kuwezesha wananchi na kutekeleza vigezo vilivyowekwa kiushindani na kufanikiwa kufikia nafasi ya pili kwa mwaka 2018.

" Ninaamini ushindi huu umetupa hamasa kimkoa ya kufanya vizuri zaidi ili mwakani tuweze kushika nafasi ya kwanza Kitaifa"alisema Sangu.Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti na mtandao huu wawakilishi wa wananchi kutoka katika vikundi, Asasi na jumuia za wafanyabiashara wameeleza kufurahishwa na juhudi zinazofanywa na Serikali ya Mkoa katika kuinua uchumi wa wananchi.

Serikali ya Mkoa wa Kigoma imeahidi kuendelea kuwawezesha wananchi katika shughuli za ujasiriamali na uanziashaji wa viwanda vidogo ili kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa Mkoani humo, ili kutoa tija zaidi katika biashar wanazofanya wajasiriamali hao.
Afisa wa dawati la uwezeshahi kiuchumi Mkoa wa Kigoma Deogratias Sangu akimkabidhi kombe la ushindi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga katika ukumbi wa utamaduni Wilayani Kasulu,kulia akishuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Brigedia Jenerali Marko Gaguti
Katibu tawala wa Mkoa wa Kigoma(RAS) Amos Charles Pallangyo akionyesha kombe ambalo Mkoa wa Kigoma umeshinda baada ya kushika nafasi ya pili Kitaifa katika kuwezesha wananchi kiuchumi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...