Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Timu ya KMC Fc imeendelea na usajili wake wa kuzidi kuimarisha kikosi chao kinachonolewa na Kocha Mrundi Etienne Ndayiragije kwa kumsajili kiungo mshambuliaji  Abdul Hillary Hassan aliyekua anakipiga katika timu ya Tusker Fc ya Nchini Kenya.

Hillary mwenye umri wa miaka 23 na refu wa futi 6 amesaini kandarasi ya mwaka mmoja kwa ajili ya kukitumikia kikosi hicho kilichopanda ligi kuu msimu wa 2018/19.

Mchezaji huyo anayetumia miguu yote kwa ufasaha amekulia katika kituo cha DYOC (Dar es saalam Youth Olimpic Centre) na msimu wa 2014-16  wa ligi kuu Tanzania Bara Aliweza kucheza  timu ya  African Lyon  kabla ya kutimkia nchini Kenya.

 Mwaka 2017, Hillary alianza kutumikia ligi kuu ya kenya na kufanikiwa kuchezea katika timu ya Tusker fc ambayo uwezo wake aliouonesha uliweza kumpa nafasi ya kuitwa timu ya taifa Kilimanjaro Stars na kushiriki michuano ya CECAFA Senior challenge cup 2017.

Mchezaji huyo ametia saini kandarisi hiyo mbele ya Meneja wa timu Walter Harrison tayari kwa kuanza kazi ya kuhakikisha KMC itaendelea kusalia katika ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Mpaka sasa KMC wamefanikiwa kunasa saini za wachezaji wazoefu wa Ligi Kuu Kama Juma Kaseja kutoka Kagera, Humud, Ally Ally kutoka  Stand United na wengineo.
Kiungo Mshambuliaji  Abdul Hillary Hassan (kulia) akiwa pamoja na Meneja wa timu ya KMC Fc Walter Harrison (Kushoto) baada ya kusaini kandarasi ya mwaka mmoja kutumikia kikosi hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...