Komredi Song Tao Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti Cha China (CPC) amewasili nchini Tanzania na kupokelewa na mamia ya wanachama wa CCM wakiongozwa na Ndg. Bashiru Ally Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.

Komredi Song Tao amefanya mazungumzo na Viongozi wa Sekretariati ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba, ambapo ameendelea kusisitiza kuwa CPC itaendeleza ushirikiano na urafiki mzuri na CCM uliosisiwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mao Zedong miaka zaidi ya 50 iliyopita.

Naye Ndg. Bashiru ally Katibu Mkuu wa CCM akimkaribisha Ndg. Tao nchini Tanzania amesema, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinathamini sana uhusiano kati ya CCM na CPC na Uhusiano mzuri sana uliopo kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya China na kwa niaba ya CCM amemhakikishia Ndg. Song kwamba ushirikiano zaidi katika Nyanja mbalimbali kwa manufaa ya vyama vyetu na wananchi wa mataifa yetu.

Komredi Song Tao yupo nchini kwa ajili ya Mkutano wa Kidunia wa vyama vya siasa utakaofanyika siku ya tarehe 17 na 18 Julai 2018, pia atashiriki katika uwekaji wa jiwe la msingi wa Chuo cha Uongozi cha Chama Cha Mapinduzi kitakachojulika kwa jina la Chuo cha Uongozi Cha Mwalimu Julius Nyerere.

Aidha, Komredi Song Tao atatembelea Chuo kikuu cha Dar es Salaam na Stesheni ya Tazara.


Ndg Song Tao Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama cha Kikomunisti cha Watu wa China akivalishwa Skafu na Vijana wa Chipukizi wa Chama cha Mapinduzi mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl Nyerere jijini Dar es salaam, Kulia kwake ni Ndg Bashiru Ally Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi.
Ndg Song Tao (Kushoto) Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama cha Kikomunisti cha Watu wa China na mwenyeji wake Ndg Bashiru Ally Kakulwa (Kulia) Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi wakikagua Gwaride maalum la vijana wa Chipukizi wa Chama cha Mapinduzi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Ndg Bashiru Ally Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Kakulwa akifanya mazungumzo na Mgeni wake Ndg Song Tao Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama cha Kikomunisti cha Watu wa China mara baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Ndg Bashiru Ally Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi akiwa na Mgeni wake Ndg Song Tao Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama cha Kikomunisti cha Watu wa China Uwanja wa Ndege wa Mwl Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...