Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii

IMEELEZWA kuwa kumkamata mtuhumiwa kabla upelelezi haujakamilika ni moja ya sababu inayosababisha kesi kushindwa kumalizika kwa wakati na kusababisha haki kupatikana kwa mhusika kwa haraka.

Hakimu Mkazi, Augustine Rwizile ambaye ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu amesema hayo leo mkoani Morogoro alipokuwa akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari za Mahakama kwa lengo la kuwasaidia kuandika habari za mahakama kwa ufasaha.

Amesema mtuhumiwa anatakiwa kukamatwa baada ya upelelezi kukamilika ndipo kesi ipelekwe mahakamani,  ili mshtakiwa akisomewa tuhuma zake basi  iweze kusikilizwa na kumalizika ndani ya muda ambao umepangwa.

"Kinachotakiwa kabla ya mtuhumiwa kufikishwa mahakamani ni kufanyika kwa upelelezi,  kukusanya ushahidi na kisha mtuhumiwa apelekwe mahakamani hapo kesi itasikilizwa kwa haraka,"amesema Hakimu Rwezile.

Ameongeza kuwa,  " sehemu kubwa hapa kwetu, tunaanza na ukamataji, mtu anakaa mahabusu na baadae ndipo anapelekwa mahakamani, akisahapelekwa huko ndiyo upelelezi unaanza jambo ambalo si sahihi, na limekuwa likilalamikiwa na  watuhumiwa kuwa wamekaa mahabusu muda mrefu bila kuletwa mahakamani, jambo hilo huchangiwa na suala la upelelezi kutokukamilika".

Ameongeza matakwa ya sheria yanataka mtuhuhumiwa akikamatwa anatakiwa kufikishwa mahakamani ndani ya saa 24.

" Ikitokea mtuhumiwa amekamata na amefikishwa mahakamani halafu akatoa malalamiko kuwa baada ya kukamatwa amekaa mahabusu kwa muda mrefu basi hakimu unatakiwa kuliangalia suala hilo kabla hajaendelea na hatua nyingine, "amesema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Habari , Elimu na Mawasiliano, Mahakama Mkuu ya Tanzania, Nurdin Ndimbe amewataka wanahabari kutumia mafunzo hayo ya siku tano kuhakikisha wanafuata sheria na taratibu za mahakama wakati wa kuripoti taarifa za mahakama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...