Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al- Najem (kanzu nyeupe) amemkabidhi Waziri wa Madini, Anjellah Kairuki misaada ya kibinadamu na vyakula tani saba vyenye thamani ya dola za marekani 8500 sawa na shilingi milioni 20 takriban kwa kaya 980 za wananchi 7,000 waliokumbwa na mafuriko katika kijiji cha Ruvu Jiungeni Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro. 

Hafla ya kukabidhi misaada hiyo iliyotolewa na Serikali ya Kuwait kwa kupitia Ubalozi wake ulipo nchini ilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemery Sinyamule, Kaimu Mkuu wa Idara ya Mashariki ya Kati kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Afrika Mashariki, Suleiman Saleh, maafisa mbalimbali wa Serikali na wananchi wa Kilimanjaro.

Akikabidhi chakula hicho ukiwemo, mchele, mahindi, maharage, sukari na mafuta ya kupikia ,  Balozi Al-Najem ameahidi kutoa misaada zaidi kwa wahanga wa mafuriko hayo yakiwemo mahema.

Naye Waziri wa  Madini, Angela Kairuki amezitaka kamati za ugawaji za ngazi zote kuhakikisha misaada hiyo inawafikia walengwa na kuahidi kuendelea kutafuta wahisani zaidi kwa kuwa wahanga hao bado mahitaji yao ni makubwa.
 Sehemu ya misaada uliyotolewa na Serikali ya Kuwait kwa kupitia Ubalozi wake ulipo nchini ikiwa tayari kugawiwa kwa walengwa, baada ya kupokelewa na Waziri wa  Madini, Angela Kairuki katika kijiji cha Ruvu Jiungeni Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...