*Simba, Mtibwa kupambana Agosti 18 katika mechi ya Ngao ya hisani

Na Khadija Seif,globu ya jamii

PAZIA la michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2018-2019 linatarajia kuanza rasmi Agosti 22 mwaka huu.

Ambapo kabla ya kuanza kwa ligi kutakuwa na mechi ya Ngao ya Hisani itakayowakutanisha Simba na Azam FC katika uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza.Mechi hiyo itachezwa Agosti 18 mwaka huu

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura amesema jumla ya timu 20 zitashiriki katika ligi hiyo huku akisisitiza ligi itaanza Agosti 22 na kumalizika Mei 29 mwakani.

Amesema kuwa  mpangilio wa ratiba umezingatia matakwa ya mdhamini mkuu ambaye ni Azam TV na  kalenda ya michuano ya kimataifa.

Amefafanua kuwa mechi katika ligi hiyo zitakuwa zinachezwa kati ya saa 8 mchana na saa nne usiku na kwamba asilimia 90 ya mechi zitachezwa kuanzia saa 12 jioni hasa katika siku za kazi.

"Tunatangaza rasmi ratiba ya Ligi Kuu msimu wa 2018-2019 ambapo jumla ya timu 20 zitashiriki kwani awali tulikuwa na timu 16 na sasa timu nne zimeongezwa,"amefafanua Wambura.

Kuhusu mtanange wa Ngao ya hisani Wambura amesema kumekuwa na kawaida kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu kunakuwa na mechi inayowakutanisha mabingwa wa Ligi kuu pamoja na bingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...