*Pia akerwa na tabia ya wahalifu kupanga ratiba, ataka kazi zifanywe saa 24


Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola ametoa maagizo kadhaa kwa idara mbalimba zilizopo chini yake kuhakikisha wanayatekeleza kwa maslahi ya nchi.

Ametoa maagizo hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anatoa tathimini ya ziara yake aliyoifanya katika vyombo vya vyote vya ulinzi na usalama na idara zote za wizara hiyo.

Amefafanua katika ziara yake aliyoianza Julai 11 mwaka huu yako mambo ambayo ameyabaini na hivyo ameona haja ya kuyaeleza kwa mustakabali wa ustawi wa Taifa kwa ujumla. “Miongoni mwa mambo ambayo nimeelekezwa na Rais Dk.John Magufuli ni kuhakikisha anasimamia suala la Magereza kujitosheleza kwa chakula.

“Hivyo nimeagiza Jeshi la Magereza nchini kuwasilisha mkakati madhubuti na unaotekelezeka wa kujitosheleza kwa chakula ili kuipunguzia Serikali mzigo wa kulisha wafungwa,”amesema.

Akifafanua katika hilo amesema kuwa kama mkakati huo kutakuwa na kipengele kinachoweka vikwazo kwa wafungwa kutofanya kazi za kuzalisha basi katika Bunge la Septemba wataanza kwa kuweka kipengele ambacho kinaelekeza wafungwa kufanya shughuli za uzalishaji chakula.

“Mbona walioko majumbani wanalima kwa ajili ya kupata chakula kwanini waliko magerezani wasilime chakula kwa ajili yao na ikiwezekana kupata na ziada kwa ajili ya kulisha maeneo mengine,”amesema.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...