THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

LUGUMI AITWA OFISINI KWA LUGOLA SAA MBILI ASUBUHI

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kuhakikisha linampeleka mmiliki wa Kampuni ya Lugumi, Said Lugumi ofisni kwake Dodoma Julai 31 mwaka huu.

Lugola ametoa maagizo hay oleo ofisni kwake jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa anamhitaji Lugumi ofisini kwake saa mbili asubuhi ya Julai 31 na kufafanua kuwa Lugumi alikuwa amepewa mkataba wa kufunga vifaa vya utambuzi wa alama za vidole baina ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kampuni yake.

“Najua Lugumi ni mtanzania mwenzetu na hivyo ninapomuhitaji najua atafika kwa wakati.Nitafurahi zaidi siku hiyo kama nikisikia mlango unagongwa na kasha baada ya kuufungua nikamuona Lugumi,”amesema Lugola.Alipoulizwa anamuitwa kwa ajili ya kitu gani akajibu ni vema ikafahamika kampuni yake ilikuwa imeingia mkataba na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, hivyo anataka kuzungumza naye.


MTAMBO WA KUTENGENEZA VITAMBULISHO VYA TAIFA

Wakati huo huo Lugola amesema ili kukamilisha mchakato wa usajili na utoaji wa vitambulisho vya Taifa ambapo amemuagiza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamalaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA) kuwalisha taarifa kamili kuhusu ununuzi wa mtambo wa kutengeneza kadi ghafi ambao bado haujaletwa.

“Katika hili namhitaji ofisni kwangu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA aje pamoja na mmiliki wa kampuni iliyopewa zabuni ya kuleta mtambo huo kwani alishapewa fedha dola milioni 14 ambazo ni sawa na Sh.bilioni 32.

“Hivyo siku hiyo nachohitaji ni kuuona mtambo au fedha zetu ambazo tutazipeleka benki tukiwa na ulinzi,”amesema.