Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa wameahidi kushirikiana katika miradi mbalimbali ya uzalishaji mali kupitia mashirika yake ya Magereza Corporation Sole na SUMA-JKT.
Hayo yamejiri wakati wa ziara ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Phaustine Kasike  alipomtembelea Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Matin Busungu ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake  za kujitambulisha kwa viongozi mbalimbali wa kitaifa tangu ateulie kuwa mkuu wa Jeshi hilo Julai13, 2018.
Katika mazungumzo yao, wakuu hao wa taasisi hizo muhimu nchini wameonesha utayari wa ushirikiano katika miradi ya ujenzi pale taasisi moja inapokuwa na miradi mikubwa inayoweza kuhitaji utaalam au nguvu ya kuweza kushirikiana.
Aidha, Meja Jenerali Busungu amesema kuwa JKT  lipo tayari kulikopesha matrekta Jeshi la Magereza wakati litakapokuwa limekamilisha  mpango wake kilimo cha kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa kama ilivyoelekezwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.
“Namshukuru sana  Meja Jenerali Busungu kwa kuonesha utayari wa kushirikiana na Jeshi la Magereza, kilichobaki ni kujipanga na kuanza utekelezaji mara moja”. Amesema Jenerali Kasike.
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akifuatilia kwa makini mazungumzo kati yake na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali, Martin Busungu(kulia) alipomtembelea Ofisini kwake leo Julai 20, 2018 jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujitambulisha rasmi tangu aapishwe rasmi kuwa Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara.
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike (kushoto) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa – JKT, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali, Martin Busungu.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa – JKT, Meja Jenerali, Martin Busungu mara baada ya mazungumzo Ofisini kwake leo Julai 20, 2018 jijini Dar es Salaam(Picha zote na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Makao Makuu ya  Jeshi la Magereza).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...