MAJAJI na Mahakimu wameshauriwa kuzingatia sheria katika utoaji haki na wafuate miiko ya kazi zao na kuhakikisha hawafanyi wanayoyataka wao.

Ushauri huo ulitolewa mapema Julai 27, jijini Dar es Salaam na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Bernard Luanda katika hafla ya kuagwa kitaaluma yeye na Jaji mstaafu wa mahakama hiyo, Sauda Mjasiri iliyofanyika katika ukumbi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.
Hafla hiyo ambayo iliongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Juma na kuhudhuriwa watu mbalimbali wakiwemo Majaji wa mahakama ya Rufani, Majaji wa Mahakama Kuu, Majaji wastaafu wa mahakama ya Rufani. 

“Kazi ya kutoa haki ni ngumu, wanapokuja watu mahakamani kila mtu anavutia upande wake, hivyo lazima utumie busara zako na sheria inasemaje,”alisema Jaji Mstaafu, Mhe.Luanda.
“Majaji na Mahakimu wazingatie sheria, katika mahakama kila hatua ni sheria, lakini siyo sheria tu imani ya wananchi kwa mahakama ni nguzo ya mahakama,” alisema na kuongeza wananchi ni muhimu kwa na imani na mahakama. 

Alisema wananchi wasipokuwa na imani na Mahakama ni hatari kwa kuwa wanaweza kujichukulia sheria mkononi.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) na Majaji wastaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Benard Luanda (wa tatu kulia) na Mhe. Sauda Mjasiri wakiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. 
Majaji Wastaafu wa Mahakama ya Rufani wakiwa katika nyuso za furaha mara baada ya kuagwa rasmi kitaaluma baada ya kustaafu kwa mujibu wa sheria, kushoto ni Mhe. Benard Luanda na kulia ni Mhe. Sauda Mjasiri, na katikati ni mke wa Mhe. Jaji Luanda. 
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (aliyeketi upande wa juu kulia) akiongoza hafla ya kuwaaga kitaaluma Majaji wastaafu wawili wa Mahakama ya Rufani waliomaliza muda wao kwa mujibu wa sheria, wa kwanza kulia ni Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Benard Luanda, na aliyeketi kushoto ni Jaji Mstaafu, Mhe. Sauda Mjasiri, walioketi mbele ya Wahe. Majaji kushoto ni Msajili, Mahakama ya Rufani, Mhe. John Kahyoza na kulia ni Mhe. Mpepo, Naibu Msajili Mahakama ya Rufani. 
Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi (aliyeketi mbele wa kwanza kushoto) pamoja na baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Watendaji na Watumishi wa Mahakama wakiwa katika sherehe ya kuwaaga Kitaaluma Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani waliostaafu kwa mujibu wa sheria. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...