Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mstaafu wa Magereza, Joel Bukuku(kulia)  akiwa kwenye gari maalum pamoja na Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mstaafu wa Magereza Deogratis Lwanga(kushoto) wakipita katikati ya Gwaride likiwa katika umbo la OMEGA ikiwa ni ishara ya kuwaaga rasmi baada ya kustaafu utumishi wao Jeshini. Hafla hiyo imefanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 13, 2018.

 Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakitoa salaam ya heshima kwa Wastaafu wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani) katika hafla ya kuwaaga wastaafu hao iliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 13, 2018.
 Makamishna Wasaidizi Waandamizi wastaafu wa Magereza wakipita wakiwapungia mikono maafisa, askari na wageni mbalimbali waliofika katika hafla ya kuwaaga wastaafu hao iliyofnyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 13, 2018.
  Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mstaafu wa Magereza Deogratis Lwanga akikagua Gwaride maalum lililoandaliwa na Maofisa na askari wa Jeshi la Magereza kwa ajili ya kuwaaga wastaafu wa Jeshi hilo..
 Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mstaafu wa Magereza, Joel Bukuku  akisalimiana na Kamishna wa Magereza, Gedion Nkana mara baada ya gwaride rasmi la kuwaaga wastaafu hao katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mstaafu wa Magereza Deogratis Lwanga(katikati) paoja na Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mstaafu wa Magereza, Joel Bukuku( wa pili kulia)  walioketi wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza waliosimama mstari wa nyuma mara baada ya hafla ya kuwaaga wastaafu hao. Wengine walioketi(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Magereza, Augustine Mboje, wa pili toka kushoto ni Kamishna wa Magereza, Hamis Ngarama na wa kwanza kulia ni Kamishna wa Magereza, Gedion Nkana
Picha zote na Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Makao Makuu ya Magereza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...