Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (mwenye tai nyekundu) akimuangalia Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba, Bw. David Elias, baada ya kumkabidhi cheti cha ushindi wa pili katika kipengele cha Wizara, Mamlaka na Wakala za Serikali zilizofanya vizuri katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Saba Saba) yaliyofungwa Jumamosi Julai 13, 2018 jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (mwenye tai nyekundu) akiwa pamoja na washindi wa nafasi ya pili na tatu ya Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa aliowakabidhi wakati wa kufunga maonesho hayo. Wengine ni Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Stella Manyanya (Mb), Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa Zanzibar, Mhe. Hamis Hafidh Hassan (mwenye tai ya blue) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara, Bw. Edwin Rutageruka (mwenye suti ya blue).
 Mwenyekiti wa Bodi Tendaji ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Esther Hellen Jason (katikati) akiwapongeza washiriki wa Maonesho kwa ushindi wa pili mara baada ya kutembelea banda la Mamlaka leo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba,        Bw. David Elias, akiwa ameshikilia zawadi ya cheti cha ushindi wa pili mara baada ya kukabidhiwa kwenye hafla ya kufunga maonesho ya Saba Saba leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Biashara, Bw. George Kasinga na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Kemikali, Bw. Christopher Anyango.

Wakurugenzi wakiwa pamoja na baadhi ya washiriki wa maonesho ya 42 ya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Saba Saba) kwa mwaka 2018 mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya ushindi wa pili kwenye hafla ya kufunga maonesho hayo Jumamosi Julai 13, 2018 kwenye viwanja vya Maonesho, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...