THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MAZOEZI SASA NI KILA WIKI Wilayani SAME mkoa wa Kilimanjaro

Hiari yashinda utumwa. Hayo ni maneno yaliyosemwa na Wana-Same baada ya kupokea taarifa inayoonyesha athari za magonjwa yasiyoambukiza ambayo mengi yanatokana na kutofanya mazoezi na kutokula vyakula sahihi. 
Mratibu wa michezo ameagizwa kupanga ratiba ya wananchi  kufanya mazoezi kila wiki baada ya wananchi hao kuagizwa kufanya mazoezi ya japo nusu saa kila siku ili vijana waonesha mwamko kuliko watu wazima. 
Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe. Rosemary Sitaki ameelekeza elimu itolewe nusu saa kila baada ya mazoezi ili kuongeza mvuto wa watu kuja kwenye mazoezi. 
Mada zenye nguvu kujadiliwa ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero kutoka kwa wananchi mbalimbali. 
Hakika " Same is not the same"
Mazoezi yaliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe. Rosemary Sitaki
Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe. Rosemary Sitaki akitoa nasaha za umuhimu wa mazoezi ya kila siku
Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe. Rosemary Sitaki akiwa na vijana waliodamka kufanya mazoezi Jumamosi