Na Frankius Cleophace, Tarime.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime  Bw. Elias Ntiruhungwa amewasimamisha kazi watumishi watatu akiwemo kaimu mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Tarime baada ya gari la wagonjwa la hospitali hiyo kukamatwa likisafirisha  dawa za kulevya aina ya mirungi wilayani Bunda mkoani Mara mnamo Julai 11, Mwaka huu.

Waliosimamishwa kazi ni Kaimu Mganga Mkuu (DM) Dkt Innocent Kweka, Kaimu Mganga Mfawidhi Dkt Amir Kombo na katibu wa Hospitali Rwegasira Karugwa kutokana na uzembe waliofanya mpaka kitendo hicho kinafanyika.

“ Namsimamisha kazi DMO, Mganga Mfawidhi na Katibu wa hospitali kuanzia leo hadi tutakapomaliza uchunguzi wetu ambao umeanza kubaini kwa nini gari la wagojnwa lilitumika kusafirisha madawa ya kulevya. Kama watabainika hawana hatia watarudi kazini”alisema Mkurugenzi huyo.

Ntiruhungwa amesema hawezi kuvumilia kitendo hicho ambacho kimechafua jina la Hamashauri yake na nchi kwa ujumla na kwamba yeyote ambaye atabainika kuhusika katika tukio hilo atachukuliwa hatua kali. 

Ameongeza kuwa tayari suala hilo linafanyiwa uchunguzi wa kina ili kubaini dereva huyo George Matai alipataje fursa ya kusafirisha madawa ya kulevya kwa kutumia gari la wagonjwa na kusema kuwa tayari amemsimamisha kazi kuanzia leo.

“Huyu dereva alichokifanya ni kitu cha kushangaza sana na cha kuaibisha Taifa kwa ujumla. Lazima afukuzwe kazi, na  kwa sasa tayari anashikiliwa na Polisi na akitoka hata kama ni baada ya Miaka 20 na kama sipo Maandishi yapo atafukuzwa tu hatuwezi fumbia macho suala hili”, alisema Mkurugenzi.

Mkurugenzi huyo aliwataka wakuu wa idara katika Halmashauri yake kutimiza wajibu wao kikamilifu ili kuepekuka vitendo vya aibu kama hivyo kutokea tena.Kamanda wa polisi Mkoa wa Mara(RPC) Juma Ndaki aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa dereva huyo na mtuhumiwa mwingine wanashikiliwa baada ya kukamatwa na shehena ya mirungi.
Mkurugenzi wa Halmshauri ya Mji wa Tarime Bw. Elias Ntiruhungwa akiongea na Vyombo vya habari katika ofisi yake ambapo amewachukulia hatua Viongozi watatu kutokana na sakata la gari la wagonjwa e kukutwa na dawa za kulevya Mirungi Viroba 34.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...