Na Mwashungi Tahir
NAIBU  Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman  alisema  matarajio ya kuwapatia  wananchi huduma zilizo bora za afya  popote walipo ndio dhamira kuu ya Wizara zote za afya za Tanzania Bara na Zanzibar.

Hayo aliyasema  leo huko katika  ukumbi wa  Ngalawa Beach Resort wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mrejesho wa maamuzi  na maazimio ya mkutano  mkuu wa 71 wa Afya Ulimwenguni  .

Alisema Huduma za afya zinahitajika  kuwafikia wananchi  hivyo ili kufikia jitihada hizi Serikali zetu mbili hizi zimepiga hatua kubwa kuhakikisha kila sehemu zinawafikia walengwa bila matatizo yeyote na kwa urahisi.

Aidha alisema baada ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 nchi yetu imekuwa ikichukuwa kila jitihada ili kufikia malengo yaliyotarajiwa , hivyo nchi yetu imekuwa ni moja kati ya nchi chache Barani Afrika , zenye mtandao mzuri wa miundo mbinu ya Afya.

Amewahakikishia wananchi kuwa sasa huduma za Afya   za msingi zinapatikana katika masafa  yasiozidi kilomita nne hadi tano  hili ni jambo jema na tunapaswa kujipongeza.
 Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Harus Said Suleiman akifungua Mkutano wa Marejesho wa Maamuzi na maazimio ya Mkutano Mkuu wa (71) wa Afya Ulimwenguni katika Ukumbi wa Hoteli ya Ngalawa Mjini Zanzibar.
 Mwakilishi wa Shirika la Afya Ulimwenguni Tanzania (WHO) Dkt. Adiele Onyeze akizungumza katika Mkutano wa Marejesho wa Maamuzi na Maazimio ya Mkutano Mkuu wa (71) wa Afya Ulimwenguni katika Ukumbi wa Hoteli ya Ngalawa Mjini Zanzibar.
 Naibu Waziri wa Afya Tanzania faustine Ndugulile, akionesha kipeperushi cha  Mpango kazi kilichoandaliwa na Wizara ya Afya Tanzania katika Mkutano wa Marejesho wa Maamuzi na Maazimio ya Mkutano Mkuu wa (71) wa Afya Ulimwenguni katika Ukumbi wa Hoteli ya Ngalawa Mjini Zanzibar.
  Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa Marejesho wa Maamuzi na Maazimio ya Mkutano Mkuu wa (71) wa Afya Ulimwenguni katika Ukumbi wa Hoteli ya Ngalawa Mjini Zanzibar.
Picha ya pamoja.
Picha na Abdalla Omar  Maelezo - Zanzibar.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...