Mchezo wa bahati nasibu wa Mojaspesho umetoa kwa mara ya kwanza mshindi wa kiasi kikubwa cha pesa cha shilingi Milioni 204 kwa ROSEMARY ONESMO LUHAMO, mfanyabiashara kutoka MPWAPWA DODOMA mwenye umri wa miaka 26.

Akuzungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi pesa kwa mshindi, Meneja biashara wa kampuni ya Lucy Games Patrick Salamouni ambayo ndio inajechezesha mchezo wa Mojaspesho alisema kuwa ushindi wa Rosemary umekuja baada ya kucheza Mojaspesho zaidi ya mara nyingi sana bila kukata tamaa, na hatimaye kulinganisha namba zake za tatu spesho ambazo zilikuwa 873 siku ya Jackpot ya Jumamosi ya tarehe 14 mwezi Julai 2018.

Huu ni mchezo wa bahati nasibu. Unaweza ukacheza mara moja ukashinda lakini pia unaweza isishinde. Ninachoweza kuwaambia ni kuwa kila mtu anayecheza anayo nafasi ya kuwa mshindi. Naomba Watanzania kuwa huu ni mchezo halali na kila anayeshinda anapata zawadi yake, alisema Salamouni. Salamouni aliongeza kuwa huu ni ushindi mkubwa kuwahi kutokea tangu Moja Spesho ianze kuchezesha Droo zake na ni uthibitisho kuwa kila mtu anaweza kushinda Mojaspesho.

‘Unaweza kucheza MOJASPESHO kupitia simu yako ya mkononi kwa kuingia sehemu ya KULIPIA BILI kwa watumiaji wa AIRTEL MONEY, TIGO PESA, MPESA au HALOPESA, kisha ingiza NAMBA YA KAMPUNI/BIASHARA ya MOJASPESHO ambayo ni 123255 - kisha INGIZA NAMBA ZAKO 3 SPESHO ZA USHINDI’ aliongeza Salamouni.

Mshindi RoseMary Onesmo Luhamo (katikati) akikabidhiwa zawadi ya ushindi wake wa milioni 204 kutoka kwa Meneja wa Lucky Games Ltd, Patrick Salamouni, ambayo ni kampuni inayochezesha mchezo wa MojaSpesho pamoja. Kushoto ni Meneja wa tawi la benki ya CRDB Azikiwe Premier Fabiola Msula.
Mshindi RoseMary Onesmo Luhamo wa kwanza wa droo ya milioni 204 ya MOJASPESHO, akifurahi baada ya kukabidhiwa pesa za ushindi wake leo jijini Dar es Salaam. Kwa kucheza mchezo wa MOJASPESHO kupitia simu yako ya mkononi nenda sehemu ya KULIPIA BILI kwa watumiaji wa AIRTEL MONEY, TIGO PESA, MPESA au HALOPESA, kisha ingiza NAMBA YA KAMPUNI/BIASHARA ya MOJASPESHO ambayo ni 123255 - kisha INGIZA NAMBA ZAKO 3 SPESHO ZA USHINDI’

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...