Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa ametembelea mradi wa uchimbaji wa visima virefu vya Kimbijii na Mpera wenye thamani ya Bilioni 19.6  vitakavyosaidia kupatikana kwa lita za maji Milioni 260 kwa siku.

Mradi huo wa visima vya maji uliochini ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) una lengo la kuongeza wingi wa maji katika maeneo mbalimbali ya Jijini Dar es Salaam na kufikia lita Milioni 720 kwa siku kufikia mwaka 2032.

Prof Mbarawa akiwa ameongozana na Kaimu Mkurugenzi wa DAWASA  Dkt Suphian Masasi ameweza kukagua visima hivyo na kuwataka wakandarasi wa mradi huo kuhakikisha unakamilika kwa wakati.

Akizungumza wakati wa kukagua visina hivyo, Prof Mbarawa amesema kuwa mradi huo utawasaidia wananchi wa Dar es Salaam kwa kuwa utasaidia upatikanaji wa maji safi na salama na yatakayotosheleza kwa matumizi yao.

" Mradi huu wa Kimbiji na Mpera utakaotoa Lita Milioni 260 kwa siku utasaidia sana wananchi wa Dar es Salaam, ukichukulia Mradi wa Ruvu Juu na Ruvu chini unatoa lita Milioni 502 kwa siku kwa ujumla wake utaleta chachu ksa wananchi kupata maji kwa uhakika,"amesema Prof Mbarawa.
WAZIRI Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa (katikati), akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi wa miradi ya maji wa kampuni ya EGIS, Dk. Charles Kaaya, kuhusu kupima urefu wa kisima kirefu katika mradi wa maji wa visima virefu vya Kimbiji, wakati akikagua mradi huo Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa DAWASA, Dk. Suphian Masasi.
 WAZIRI Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa  akinywa maji katika moja ya Kisima ya miradi ya maji ya Kimbiji na Mpera wakati akikagua mradi huo Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa DAWASA, Dk. Suphian Masasi.
 WAZIRI Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa akiwa pamoja Kaimu Mkurugenzi wa DAWASA, Dk. Suphian Masasikatika mradi wa maji wa visima virefu vya Kimbiji, wakati akikagua mradi huo Dar es Salaam utakaofanikisha upatikanaji wa lita Milioni 260 kwa siku.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...