Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa ametembelea Mkoa wa Shinyanga pamoja na Wilaya ya Kahama na vituo vya afya kwa nia ya kuangalia shughuli zinazofanywa na wauguzi na wakunga wa kada mbalimbali pia kuzungumza nao.

Msajili alikutana na baadhi ya wauguzi katika vituo vyao vya kazi na kuwasisitizia kuzingatia maadili wanapowahudumia wagonjwa. Pia, alifanya mkutano Mjini Kahama katika Hospitali ya wilaya na aliwakumbusha wauguzi na wakunga juu ya majukumu ya Baraza la Uuguzi na Ukunga pamoja na Misingi ya utoaji huduma ya Uuguzi na Ukunga yaani (Professional code of conduct, the guiding principles).

Katika hatua nyingine, aliwataka wauguzi na wakunga kuwa na leseni inayowaruhusu kutoa huduma, lakini pia alikemea vikali watu wanaoghushi vyeti na leseni za uuguzi na ukunga.Msajili alipata nafasi ya kujibu maswali mbalimbali ya kiutendaji pamoja na sheria inayoongoza taaluma ya uuguzi na ukunga.

Pia, alitembelea pia Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga na kuonana na wauguzi na wakunga katika maeneo yao ya kutolea huduma na kujibu maswali mbalimbali yanayohusu taaluma ya uuguzi na ukunga, sheria inayoongoza taalama ya uuguzi na ukunga nchini.
Msajili Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa akiwa ziarani mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuzungumza na wauguzi pamoja na wakunga kuhusu utoaji wa huduma bora.
Wauguzi na wakunga wa Wilaya ya Kahama wakijiandaa kumsikiliza Msajili Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agness Mtawa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...