Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii anawakaribisha wahitimu wote wa kidato cha sita na kidato cha Nne pamoja na wazazi wa wahitimu kwenye banda la Taasisi hiyo katika maonyesho ya 13 ya vyuo vikuu kwenye viwanja vya Mnazi mmoja, kukutana na wahadhiri wa taasisi na kupata maelezo ya kina kuhusu programu za masomo zitolewazo na Taasisi hiyo pia kupata maelezo ya jinsi ya kujiunga na Taasisi kwa mwaka huu wa maosmo 2018/2019 ambapo mwanafunzi atafanyiwa usajili papo hapo katika banda la Taasisi ya Ustawi wa jamii.

Ili kusajiliwa mwanafunzi afike na Vivuli vya vyeti vya kitaaluma na cheti cha kuzaliwa pamoja na ada a Usajili ambayo ni Tsh. elfu 10,000/ tu. 
Mhadhiri msaidizi wa idara ya Rasilimali watu Bi. Christina fille akitoa maelezo na kujibu maswali kwa wanafunzi mbali mbali waliofika kwenye Banda la Taasisi ya Ustawi wa Jamii. 
Wanafunzi na Wananchi mbali mbali wakipata maelezo kutoka kwa watumishi wa Taasisi ya Ustawi wa jamii kwenye maonyesho ya 13 ya Vyuo vikuu katika viwanja vya Mnazi mmoja Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...