Na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii

MWENGE wa Uhuru unatarajiwa kuzindua miradi mbalimbali katika Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani yenye zaidi ya Sh. bilioni 2.9.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filibeto Sanga wakati alipokuwa akisoma taarifa ya Wilaya hiyo ya miradi ya Maendeleo wakati wa Mwenge huo ukiwa wilayani hapo.

"Miradi itazinduliwa katika mwenge huu na imetekelezwa kwa nguvu za wananchi. Katika kuchangia nguvu zao,Serikali kuu kutuwezesha fedha ikiwamo na wadau wa maendeleo," amesema.Aliongeza kuwa miradi hiyo ya maendeleo itasimamiwa vizuri ili kuwawezesha wananchi kunufaika nayo.Pia amesema miradi yote ipo katika ubora na imesimamiwa kikamilifu kutokana na fedha zilizotolewa kwa ajili ya miradi hiyo.

Akizungumza kuhusu elimu amesema kuwa,Wilaya imejikita katika kusimamia suala la elimu ambapo idadi ya wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza na chekechea inaongezeka kila mwaka.Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Everist Ndikilo amesema kuwa Mkoa huo una wilaya saba ambapo miradi ya maendeleo yenye zaidi ya thamani ya shilingi bilioni 162 itazinduliwa katika mbio hizo za mwenge.

Ndikilo aliyasema hayo wakati akikabidhiwa mwenge na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda.Ndikilo alikabidhiwa Mwenge na Makonda,katika kijiji cha Kipara Mpakani kilichopo Mkuranga.Ndikilo amesema atahakikisha wakimbiza mwenge wote sita wanakaa kwa usalama katika Mkoa huo.
 Mku wa Mkoa wa Pwani Muhandisi,Everist Ndikilo  akimkabidhi mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga.(picha na Emmanuel Massaka MMG)
 Kiongozi wa  mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018,Ndugu  Charles Kabeho akiweka jiwe la msingi katika kituo cha Afya Mkamba kilichopo kijiji cha Kizapala  Mkuranga  mkoa wa Pwani,kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mh.Abdallah Ulega .
 Kiongozi wa  mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018,Ndugu  Charles Kabeho akifungua vyumba sita vya vya madarasa ya shule ya msingi Kipara mpakani Mkuranga  mkoa wa Pwani.(picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega  akizungumza na wananchi wa waliojotokeza kwa wingi kuupokea Mwenge wa Uhuru.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...