Na Kumbuka Ndatta,Arusha

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalla Ulega ametembele taasisi za Serikali zilizopo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na wadau wengine wa sekta ya mifugo na uvuvi.

Akitoa taarifa fupi kwa Naibu waziri,Mkurugenzi wa Wakala wa vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA) Kampasi ya Tengeru Joseph Msemwa amemweleza Ulega kuwa kazi kubwa ya LITA ni kutoa mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi,kufanya utafiti na ushauri elekezi na uzalishaji Mali.

Pia mafunzo hayo yamejikita katika fani ya afya ya mifugo na uzalishaji.Aidha mafunzo hayo yanalenga kutoa watalaam wenye ujuzi wa hali ya juu katika fani za ufugaji.Amesema lengo ni kuwa na mtazamo wa Kujiajiri na kuendesha miradi mbalimbali ya kibiashara.

Msemwa amemwambia Naibu Waziri baadhi ya changamoto zinazoikabili Kampasi hiyo kuwa ni uchakavu wa majengo,huduma duni za maji,upungu wa watumishi na Muundo wa Wakala.Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa LITA (CEO)Magreth Pallangyo pamoja na kupokea maagizo kutoka kwa Naibu Waziri,ameahidi kuyatekeleza maagizo yote yaliyotolewa na kuyashughukia ipasavyo.

Akihutubia watumishi waliofika katika ukumbi wa Kampasi ya Tengeru Ulega amesema kuwa vyuo hivi vya mafunzo ya mifugo ndio nguzo mama katika kuchochea maendeleo ya uchumi wa Taifa letu."Wakufunzi wa Vyuo hivi vya Mifugo jitahidi sana kuhusianisha kile mnachokifundisha darasani na mazingira halisi ya itanzania.

"Toeni elimu bora ili muweze kuwasaidia vijana hawa na taifa kwa ujumla.Vijana hawa wakitoka hapa tunataka waone kuwa wamezungukwa na fursa za kiuchumi," amesema Ulega.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiangalia ng`ombe wa uhimilishaji katika kituo cha Taifa cha(NAIC) kilichpo Usa River jijini Arusha.
 Mkufunzi mwandamizi wa kitengo cha teknolojia ya maziwa,Theresia Teti  akimwelezea  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega namna ya usindikaji wa maziwa jijini Arusha.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiangalia namna ya uhimilishaji unavyofanyoka katika kituo cha Taifa cha(NAIC) kilichopo Usa River jijini Arusha.Picha na Emmanuel Massaka,MMG Arusha)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akitembelea shamba la samaki Shazan lililopo jijini Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...