Mgunduzi wa Madini ya Tanzanite Mzee Jumanne Mhero Ngoma, ambaye anasumbuliwa na maradhi ya kupooza mwili,  leo amenza matibabu katika Hospitali ya Apollo jijini New Delhi nchini India.
Kwa mujibu wa binti yake, Bi. Asha Ngoma, mgunduzi huyo ameamua kusaka matibabu zaidi  baada ya kufanyiwa matibabu ili kuona kama anaweza kupona kwa uharaka zaidi.
“Mzee amekuwa akipatiwa matibabu tokea wakati ule Rais Magufuli  alipomzawadia pesa shilingi milioni 100 mwezi wa Aprili mwaka huu  ya matibabu wakati  uzinduzi wa ukuta unaozunguka machimbo ya madini Mirerani mwezi April mwaka huu.
“Tunamshukur sana Rais Magufuli kwani pesa hiyo tulipewa mara moja nasi tukaanza matibabu hapo nyumbani  na kwa kweli amemsaidia sana sana  na hapa India tunatarajia matibabu yatamsaidia zaidi”, alisema Bi. Asha ambaye ameongozana  na mjukuu wa Mzee Ngoma, Khalifa. 
 Mgunduzi wa Madini ya Tanzanite Mzee Jumanne Mhero Ngoma akipokewa na muuguzi leo tayari kupelekwa kuanza matibabu katika Hospitali ya Apollo jijini New Delhi nchini India. Pamoja naye ni bintiye, Asha Ngoma na mjukukuu, Khalifa
 Mgunduzi wa Madini ya Tanzanite Mzee Jumanne Mhero Ngoma akiwa kwa daktari baada ya kupokelewa katika Hospitali ya Apollo jijini New Delhi nchini India. Pamoja naye ni bintiye, Asha Ngoma na mjukukuu, Khalifa
 Mgunduzi wa Madini ya Tanzanite Mzee Jumanne Mhero Ngoma akiingizwa wodini tayari kuanza matibabu katika Hospitali ya Apollo jijini New Delhi nchini India. 
Daktari wa zamu akimpima Mgunduzi wa Madini ya Tanzanite Mzee Jumanne Mhero Ngoma mara tu baada ya kufikishwa wodini katika Hospitali ya Apollo jijini New Delhi nchini India. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...