Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kagera

MFUKO wa Taifa wa Bima ya afya(NHIF) Mkoa wa Kagera wamekabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi wanaosaidia wazee katika kituo cha kulelea wazee cha kilima kilichopo halmashauri ya Wilaya ya Bukoba. 

Meneja wa mfuko wa bima ya afya(NHIF)Kagera Elias Odhiambo alisema kuwa huo ni utekelezaji wa ahadi ilitolewa na mfuko katika harambee ya kuchangisha fedha na vifaa vya ujenzi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi kwenye kituo cha kulelea wazee cha kiilima ambazo ziliathiriwa na tetemeko la ardhi ambapo harambee hiyo iliendeshwa na Naibu Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia na watoto Faustine Andungulile.

"NHIF leo tumetimiza ahadi yetu tuliyotoa ya kutoa msaada wa vifaa vya ujenzi kwaajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi katika kituo hiki,hii ni sehemu ya misaada inayotolewa na mfuko kusaidia jamii katika shughuli mbalimbali za maendeleo,naamini msaada huu utasaidia ujenzi wa makazi haya"alisema

Odhiambo alisema vifaa walivyokabidhi ni mifuko 100 ya sementi na mabati 50 vifaa hivyo vyote vinathamani ya shilingi 3,100,000.Baada ya kupokea msaada huo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu aliushukuru uongozi wa mfuko wa bima ya afya(NHIF)kwa kutimiza ahadi yao waliyo haidi kwa wakati.

"Meneja ninakuomba nifikishie shukrani zangu kwa Mkurugenzi mkuu wa mfuko mmetekeleza ahadi yenu mliyotoa ndani ya wakati ili kufanikisha zoezi hili la ujenzi"alisema.Kijuu aliwataka wakandarasi kuhakikisha ujenzi unafanyika kwa kasi na kukamilika kwa wakati aliwaomba pia wadau wengine kuendelea kutoa misaada ili ujenzi huo uweze kukamilika.
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali  Mstaafu Salum Kijuu  akipokea vifaa vya ujenzi ikiwemo saluji na mabati kutoka kwa Meneja wa mfuko wa bima ya afya (NHIF) Kagera Elias Odhiambo kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Kulelea Wazee 
  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu  akiwasalimia baaddhi ya Wazee walioko kwenye kituo chao  
Sehemu ya ujenzi wa kituo hicho ukiendelea

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...